03 October 2013

TRENI YA MWAKYEMBE YAPATA AJALI DAR  
 Baadhi ya wakazi wa jijini wakiangalia gari aina ya Scania lenye namba za usajili T 124 ATG lililo gongwana Treni ya abiria inayo fanya ruti kati ya Ubungo na Stesheni, eneo la Tazara Dar es Salaam jana. Garihilo lilikuwa limebeba chupa tupu za soda

Na Godfrey Ismaely

  Watu kadhaa ambao walikuwa wanasafiria treni ya jioni jijini Dar es Salaam wamenusurika kifo baada ya treni hiyo kugongwa na lori.


Tukio hilo lilitokea jana katika eneo la Tazara Buguruni lililopo Manispaa ya Ilala, wakati treni hiyo ya saa 12 jioni ilipokuwa inatokea katikati ya Jiji la Dar es Salaam (Stesheni ya Treni) kuelekea eneo la Ubungo Maziwa jijini humo.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, walilieleza Majira kuwa, ajali hiyo ilitokea baada ya lori namba T 124 ATG aina ya Toyota Scania ambalo lilikuwa limeegeshwa katikati ya reli kuigonga treni, hivyo kusababisha safari za treni kuishia hapo.

"Watanzania tumekosa ustaarabu kabisa, kila siku tunajua wazi kuwa hii reli huwa inatumika na treni, lakini leo (jana) unamkuta mtu ameegesha gari katikati ya reli. Tunaiomba Serikali iweke sheria kali za kuwabana hawa watu wazembe wanaotaka kuua mamia ya watu," alisema Mkazi wa Buguruni aliyejitambulisha kwa jina la Mama Mussa.

  Gazeti hili lilishuhudia lori hilo ambalo liligonga treni likiwa limedondoka ambapo lilijazwa chupa za soda, ingawa hadi tunatoka sehemu ya tukio hamna mtu yeyote ambaye alionekana kuumia kwa kuwa dereva na kondakta wa lori hilo waliruka na kukimbia.

  Usafiri huo wa treni maarufu kwa jina la Treni ya Mwakyembe ulizinduliwa rasmi na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe mwishoni mwa mwaka jana ambapo lengo ni kuhakikisha inahudumia wananchi kwa gharama nafuu jijini

2 comments:

  1. Toyota Scania ni gari jipya au mimi ndio silijui

    ReplyDelete
  2. Ni lini wa TZ tutaheshimu taratibu na kuwa wastaarabu . Hata hivo serikali ingeboresha maisha ya MTZ huenda watu wangestaarabika . maskiiiiiiini mwakyembeee ! a a a h h.

    ReplyDelete