02 October 2013

MECHI ZA SIMBA, YANGA ZAINGIZA MIL. 182/-



Na Fatuma Rashid
  Mechi za Ligi Kuu ya Vodacom zilizochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, timu za Yanga na Simba zimeingiza jumla ya sh. milioni 182.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema Yanga katika mechi yake dhidi ya Ruvu Shooting iliyochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 imeingiza sh. 94,202,000.

  Wambura alisema katika mechi hiyo, jumla ya watazamaji 16,492 walikata tiketi kushuhudia pambano hilo ambapo kila klabu ilipata mgawo wa sh. 22,630,921.58.Alisema viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000, na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 14,369,796.61.
Alisema katika mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 11,507,248.26, tiketi sh. 3,117,215, gharama za mechi sh. 6,904,348.96."Kamati ya Ligi sh. 6,904,348.96, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,452,174.48 na pia Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,685,024.59," alisema.
   Wambura alisema katika mechi ya Simba na JKT Ruvu iliyochezwa Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 87,901,000, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.Aliema watazamaji waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo walikuwa 15,780 na viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 21,051,025.92 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 13,408,627.12.
 "Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 10,703,911.48, tiketi sh. 3,132,963, gharama za mechi sh. 6,422,346.89, Kamati ya Ligi sh. 6,422,346.89."Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,211,173.44, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,248,789.67 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 1,248,789.67," alisema.
   Wakati huo huo, Wambura alisema mechi ya ligi hiyo kati ya Mbeya City na Coastal Union, iliyochezwa Jumamosi Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya imeingiza sh. 16,959,000 huku kila klabu ikipata sh. 4,035,229.
  Alisema mgawo wa mechi hiyo ulipelekwa kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 2,586,966, uwanja sh. 2,051,811.57, tiketi sh. 696,290, gharama za mechi sh. 1,231,086,       Kamati ya Ligi sh. 1,231,086, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 615,543, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA) sh. 478,756

No comments:

Post a Comment