05 September 2013

WAZIRI MKUU AAGANA NA BALOZI WA MAREKANI



Na Mwandishi Maalum
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda, amesema Tanzania itasimamia vizuri miradi iliyoanzishwa chini ya ufadhili wa Serikali ya Marekani na kuhakikisha inakamilika ili iweze kuwanufaisha wananchi waishio
kwenye maeneo ya hiyo miradi.
 Alitoa kauli hiyo juzi wakati alipokutana na Balozi wa Marekani anayemaliza muda wake hapa nchini, Alfonso Lenhardt, ofi sini kwake Bungeni, mjini Dodoma. Waziri Mkuu alimshukuru Balozi huyo kwa kuiwezesha Tanzania kunufaika na miradi mingi ya kimaendeleo katika kipindi ambacho balozi huyo amekuwa chini ya uongozi wake. 
Alisema Serikali inapitia upya miradi ya barabara iliyo chini ya MCC ili iweze kunufaisha wakazi wa vijijini kwa kufungua maeneo yao kiuchumi na kuwawezesha kupata masoko kwa urahisi. Alisema mbali ya barabara, Serikali pia imepania kuboresha upatikanaji wa umeme vijijini na wilayani ili kuwezesha uanzishaji wa viwanda vidogo vya usindikaji.“Lakini jambo hili haliwezi kufanikiwa kama sekta binafsi haitakuwa na mchango mkubwa katika suala hili,” alisema Waziri Mkuu. Marekani imeisaidia Tanzania kwenye miradi ya kuongeza lishe kwenye chakula, kupambana na malaria, afya ya mama na mtoto, UKIMWI, kilimo, barabara na nishati. 
Kwa upande wake, Balozi Lenhardt alimweleza Waziri Mkuu kwamba amefurahia kipindi chote cha miaka minne ambacho yeye na mke wake waliishi nchini na kwamba anaamini Serikali ya Tanzania itahakikisha miradi yote inayofadhiliwa na nchi hiyo, inakamilika. Alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba miradi yote iliyoanzishwa chini ya uongozi wake itakamilika na kwamba ana hakika kwamba upatikanaji wake wa fedha hautatetereka kwa sababu yeye anaondoka nchini.
 Alisisitiza haja ya sekta binafsi nchini kuhakikisha inashirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Alimkabidhi Waziri Mkuu zawadi ya sarafu maalum (coin of excellence) ambayo hutolewa kwa watu ambao utendaji kazi wao umetia fora na kumweleza kwamba anatambua mcha

No comments:

Post a Comment