02 September 2013

WAZIRI CHIZA ATAKA BODI ZA MAZAO KUSAIDIA WAKULIMA


Na Cornary Anthony, Dodoma
BODI zote na taasisi za mazao nchini zimetakiwa kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayowakabili wakulima katika maeneo husika na sio kujihusisha zaidi na mazao ya biashara.Hayo yalisemwa na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, wakati akifungua Mkutano wa wadau wa korosho mkoani Dodoma juzi.

Chiza alisema kuwa jukumu la kila bodi la zao la korosho ni kutatua changamoto zote zinazokabili zao hilo kuanzia kwenye kilimo mpaka kwenye soko. “Haifurahishwi kumuona mkulima ana mazao ya kudumu lakini hayaleti tija kwa mkulima,”alisema ChizaAlisema wameona katika Mikoa ya Mbeya, Kagera na Kilimanjaro wana mazao ya kudumu ya migomba lakini uchumi wake umeimarika sio kama zao la korosho kwani haliko kama zao la migomba.
Hata hivyo, alisema kuwa anaziomba bodi zote za mazao nchini yaani mazao ya korosho, pamba, kahawa na Tumbaku zifuate njia za mkato ya kuweza kutatua matatizo ya wananchi na si vinginevyo.Aidha aliwataka wanunuzi wa korosho nchini wasipende kuwatumia wawakilishi maana kila wanapohitaji taarifa zozote wanasema wao sio wazungumzaji. Aliipongeza Bodi ya Korosho Tanzania kwa kuweza kuongeza wataalamu katika mikoa na Wilaya ambapo hapo awali zilitokea Wilaya 34 hadi sasa zimefika 42 kwamba huo ni mwanzo.
Kwa u p a n d e wa k e Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania, Anna Abdallah, aliiomba Serikali kuunga mkono Bodi ya Korosho kwa mkakati wake wa kuwaongezea uwezo wakulima ikiwa ni pamoja na kuwafungulia viwanda vidogo na vikubwa kwa ajili ya ubanguaji korosho.

No comments:

Post a Comment