02 September 2013

TBS YAONYA WAAGIZA BIDHAA KUTOKA NJE Na Rachel Balama
SHIRIKA l a Viwa n g o nchini limewatahadharisha waingizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi kwamba bidhaa watakazoingiza wahakikishe kwamba zimekidhi viwango vinginevyo zitarudishwa zilikotoka.Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Joseph Masikitiko, wakati alipokuwa akikabidhi leseni na vyeti vya ubora kwa wazalishaji mbalimbali baada ya kukamilika kwa taratibu za udhibiti ubora.

"Mwito wangu ni kwamba waingizaji wote wa bidhaa kutoka nje ya nchi wanatakiwa kuhakikisha bidhaa hizo zimekidhi viwango, tofauti na hapo watatozwa faini na kisha bidhaa hizo zitarudishwa nje ya nchi," alisema.Alisema mpango wa kukagua bidhaa za nje ya nchi kabla ya kuletwa nchini unaendelea kuimarika, wakati TBS ikiendelea kuhakikisha bidhaa za ndani zinakidhi viwango. Alisisitiza kuwa waagizaji wa bidhaa toka nje ya nchi wanawajibika kuhakikisha bidhaa wanazoleta nchini zina ubora unaostahili.
Alisema mbali na kuwa na ubora unaostahili pia bidhaa hizo ziwe zimekaguliwa na kupewa vyeti vya ubora yaani vinavyotolewa na mawakala walioidhinishwa na shirika hilo.Alisema utaratibu wa kutoa adhabu utaendelea kwa wale wote wanaokiuka utaratibu huo ambapo kwa upande wa wakaguzi wa nje ambao hutoa vyeti bila kukagua bidhaa wakibainika mikataba itafutwa ili kuifanya Tanzania kuwa soko la bidhaa bora.
Masikitiko, aliongeza kuwa shirika linaendelea kusisitiza kwamba wazalishaji wote wa bidhaa ambazo viwango vyake ni vya lazima, vikiwemo vyakula kujitokeza kwa hiari kuthibitisha ubora wa bidhaa zao badala ya kusubiri shuruti inayoendana na kufungwa kwa viwanda vyao.
P i a a l i t o a mwi t o kwa wajasiriamali wadogo kutumia fursa ya elimu itolewayo na shirika kwa namna mbalimbali kwani moja ya majukumu ya TBS ni kuwafundisha wazalishaji kuhusu njia bora za usindikaji na kufikia viwango.Shirika hilo lilitoa jumla ya leseni na vyeti vya ubora 43 kwa bidhaa mbalimbali baada ya kukamilika kwa taratibu za kukidhi viwango vya TBS.

No comments:

Post a Comment