Na Esther Macha, Mbeya
MBUNGE wa Rungwe Mashariki, mkoani
Mbeya, Profesa David Mwakyusa, amewataka waumini wa Kanisa la Wasabato jijini
humo, kuacha tabia ya kunung'unika wanapotoa michango inayokwenda kusaidia
shughuli mbalimbali za kusaidia jamii
.Alisema baadhi ya waumini wamekuwa na
moyo wa kujitolea wanapoombwa kufanya hivyo na makanisa yao kwani kazi ya Mungu
ni kujitolea hivyo si busara kujutia ulichokitoa.
Prof. David Mwakyusa, aliyasema hayo
hivi karibuni katika harambee ya ujenzi wa Kanisa la Wasabato, lililopo katika
Kata ya Ntokela, Wilaya ya Rungwe, jijini humo.
"Ninachofahamu ni kwamba, muumini
aliyeamua kujitoa ajitoe kwa nafsi yake mwenyewe si kwa shingo upande, naomba
tubadilike kwani baadhi yetu wanaishi katika nyumba nzuri hivyo hivyo tunapaswa
kujenga kanisa lililo bora," alisema.
Akisoma risala kwa mgeni rasmi, Mjumbe
wa Kamati ya Maandalizi ya harambee hiyo, Bw. Awadi Mwandandila, alisema
wameanzisha ujenzi wa kanisa hilo kutokana na wingi wa waumini ambao hivi sasa
wanafikia 835.
Alisema ujenzi huo ulianza mwaka 2002
ambapo fedha zilizotumika hadi sasa ni sh. milioni 279 na zinazohitajika ili
kukamilisha ujenzi huo ni sh. milioni 90.
Ka t i k a h a r amb e e h i y o ,
zilipatikana sh. milioni 46 ambapo zile zilizochangwa papo kwa papo sh. milioni
23, ahadi sh. milioni 23 na Prof. Mwakyusa na familia yake walichangia zaidi ya
sh. milioni mbili.
No comments:
Post a Comment