Na Rose Itono
SHULE ya Sekondari ya St.Matthew’s
iliyoko Mk o a wa Pwa n i imetenga sh. milioni 350 kwa ajili ya motisha kwa
walimu na wanafunzi watakaofanya vizuri kwa mwaka ujao katika mitihani yao ya
mwisho ili kufanikisha mpango mkakati wa Matokeo Makubwa Sasa.
Akizungumza
katika mahafali ya 13 ya kidato cha nne shuleni hapo mwishoni mwa wiki,Mkuu wa
shule, Abrahamu Shafuri, alisema kuwa, baada ya serikali kuzindua mpango
mkakati wa maendeleo unaoitwa Matokeo Makubwa Sasa, shule yake imeajipanga
kuhakikisha inaboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Alisema kwa
mwaka huu shule ilitenga sh.milioni 306.6 kama motisha ya walimu,wanafunzi na
wazazi kwani kufanya hivyo ni chachu ya mafanikio katika taaluma na kuamini kuwa
kiasi hicho kitaleta ari na morali kwa watendaji ili kupata matokeo mazuri.
Alifafanua na
kusema kuwa jumla ya sh. milioni 256 zitawezesha kuwasafirisha walimu nje ya
nchi kwa ajili ya ziara za mafunzo ambapo pia wataweza kubadilishana uzoefu na
kujifunza mbinu mbalimbali za kufundishia.
“Motisha za
walimu na wanafunzi watakaofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha sita shule
imetenga sh.milioni 20.2, kidato cha nne, sh. milioni 16.1 na kidato cha pili
sh.14,246,”,alisema.
Naye Mkurugenzi
wa shule hiyo, Thadeus Mutembei, alisema ili kufanikiwa katika malengo hayo
wadau wa elimu wanatakiwa kubadili mtazamo wa matokeo makubwa sasa kwa
kujiuliza wanachangiaje matokeo haya.
“ I l i k u f a n i k i w a k a t i k a
ma l e n g o y e t u tuliyojiwekea,tunahitaji wadau wetu wote kubadili mitazamo
na kuwa na matazamo wa ‘Matokeo Makubwa Sasa,” alisema n a k u o n g e z a k u
w a wadau hao ni pamoja na shule,wazazi,walimu na wanafunzi.
Mutembei alisisitiza kuwa wanafunzi wa shule
hiyo kuongeza jitihada ili kujiandaa vyema na mtihani wa taifa kwa kuendelea
kumtumainia Mungu siku zote, kushirikiana na walimu pamoja na wanafunzi
No comments:
Post a Comment