Na Elizabeth Joseph,
Mpwapwa
JUMLA ya wanakijiji 29 katika Kijiji cha
Kinusi kilichopo Kata ya Ipera Wilaya ya Mpwapwa wamelipwa fidia kupisha
uchimbaji wa madini katika eneo la Mlima Kitonge kijijini hapo.A k i z u n g u
m z a k a t i k a makabidhiano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya C.S.N
inayojishughulisha na uchimbaji wa madini aina ya shaba katika eneo hilo, Juma
Chibaya alisema jumla ya shilingi milioni 89 zimetolewa na kampuni hiyo kwa
ajili ya kuwalipa fidia wanakijiji hao
.Chibaya alibainisha
kuwa kitendo cha kuwalipa fidia wananchi hao ni moja kati ya makubaliano
waliyopewa kuyafanya kabla ya kuanza shughuli ya uchimbaji huo ambapo kati ya
hao 29, 22 ni wale waliokuwa na mashamba na saba ni waliokuwa na makaburi
katika eneo hilo.Naye Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Bodi
ya Wakurugenzi katika kampuni hiyo, Cleopa Simule alisema kuwa mkataba wao
katika eneo hilo ni miaka kumi ambapo tofauti na kuwalipa fidia wananchi hao
pia kampuni yao inatakiwa kujihusisha katika shughuli nyingine za kijamii
kijijini hapo ambapo hivi karibuni inatarajia kutoa madawati mia moja kwa ajili
ya shule za msingi katika Kata hiyo.
"Mkataba wetu ni wa miaka kumi
katika uchimbaji wa madini hayo hivyo katika kipindi hicho tumekubaliana pia
kuhusika katika shughuli mbalimbali za kijamii na hivi karibuni tunatarajia
kutoa madawati mia moja katika shule za msingi zilizopo katika kata hii ambapo
awali tuliambiwa kuwa ndio changamoto kubwa inayowakabili walimu na wanafunzi
katika kata hii," alisema Simule.Aidha
alieleza kuwa bado kuna uelewa mdogo kwa wananchi juu ya sheria ya madini
kwakuwa wengi wao wamekuwa wakikataa kulipwa fidia kwa madai kuwa hazilingani
na madini yatakayopatikana katika maeneo wanayoyapisha.
No comments:
Post a Comment