PRETORIA,
Afrika Kusini
RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson
Mandela, ameruhusiwa kutoka hospitali na amekwenda kupumzika nyumbani kwake
mjini Johannesburg.Kwa mujibu wa tovuti ya ofisi ya rais
Afrika Kusini, Mzee Mandela anaendelea kuwa chini ya uangalizi maalum
Tangazo hilo limekuja siku moja baada ya maofisa
kukanusha taarifa kwamba Mzee Mandela (95), alikuwa tayari amekwisharuhusiwa
kutoka hospitali.Taarifa inasema kiongozi huyo wa zamani
wa Afrika Kusini bado yuko mahututi na wakati mwingine hali yake kiafya
inaimarika.
Mzee Mandela, rais wa kwanza wa Afrika
Kusini kuchaguliwa kidemokrasia, alikuwepo hospitali tangu Juni akipata
matibabu ya maambukizo kwenye mapafu yake.Mshindi huyo wa Tuzo ya Amani ya Nobel
anapewa heshima duniani kote kwa kuongoza mapambano dhidi ya utawala wa Wazungu
wachache na kutangaza maridhiano na jamii ya Wazungu pamoja na kufungwa jela
kwa miaka 27.
"Timu ya madaktari wake
inashawishika kwamba Mzee Mandela atapokea kiwango kilekile cha uangalizi
maalum nyumbani kwake Houghton kama alivyopokea mjini Pretoria (hospitali)," ilisema taarifa
ya Ofisi ya Rais.
Taarifa hiyo inasema nyumba yake
iliyopo katika kitongoji cha Houghton "imefanyiwa marekebisho kumruhusu
kupokea uangalizi maalum" na atatibiwa na madaktari walewale ambao
wamekuwa wakimuangalia tangu Juni 8.Kwa mujibu wa BBC, kama ikibidi, Mzee
Mandela atalazwa tena hospitali, taarifa hiyo ilisema.
No comments:
Post a Comment