Na Mwandishi Wetu
MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati
ya Simba na Mtibwa Sugar iliyochezwa juzi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
imeingiza sh. 95,080,000.Katika mechi hiyo, Simba ilitoka kifua
mbele baada ya kuifunga Mtibwa mabao 2-0
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana
kwa vyombo vya habari na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Boniface Wambura, watazamaji 16,507 walikata tiketi kushuhudia mechi
hiyo.
Alisema viingilio katika mechi hiyo
vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata
mgawo wa sh. 23,018,077.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa
ni sh. 14,503,728.81.
Wambura alisema mgawo mwingine wa
mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 11,704,107.18, tiketi sh. 2,548,890."Gharama za mechi sh. 7,022,464.31, Kamati ya Ligi sh.
7,022,464.31, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,511,232.15 na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,730,958.34,"
alisema.
No comments:
Post a Comment