16 September 2013

PINDA KORTINI LEO  •  ZAIDI YA MAWAKILI 20 KUWAKILISHA LHRC


Na Rachel Balama
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo inatarajia kuanza kusikiliza kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) pamoja na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) dhidi ya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda.

Katika kesi hiyo, Jaji Kiongozi F a k h i J a n d u , a n a t a r a j iwa kuongoza jopo la Majaji wawili ambao watasikiliza kesi hiyo, Jaji Augustine Mwarija na Jaji Dkt. Fauz Twaib.LHRC na TLS walifungua kesi hiyo dhidi ya Bw. Pinda, wakidai alitoa kauli ya kuruhusu vyombo vya usalama kuwapiga watu wanaokataa kutii sheria zinazotolewa na mamlaka husika akiwa bungeni Mjini Dodoma.
Mbali na Bw. Pinda, mwingine aliyeunganishwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ambapo upande wa LHRC unawakilishwa na mawakili zaidi ya 20.Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Bw. Pinda, anakabiliwa na tuhuma za kudaiwa kuvunja Katiba ya nchi kwa kuruhusu askari kuwapiga wananchi.
LHRC imepata saini za wananchi 2,029 wanaopinga kauli ya Bw. Pinda na kuunga mkono kufunguliwa kwa kesi hiyo.Mkurugenzi wa LHRC, Dkt. Hellen KijoBisimba, alisema Bw. amekiuka kifungu cha Katiba ya nchi Ibara 13 (1).

1 comment:

  1. Hongera wanasheria mmepata dili. Pongezi Pinda tangu kauli yako uitoe bungeni hawajajitokeza. Kumekua na utalivu. Kauli yako ina tija. Ndiyo seri'kali' tunayoitaka. Sio ya kuogopaogopa. Kwani nini? Si wanajitakia umaarufu na kutaka ripoti nzuri za kuwaridhisha wafadhili wao?

    ReplyDelete