02 September 2013

MBUNGE AWAPATIA WANAHABARI MSAADAKIKUNDI cha Waandishi wa Habari Wajasiriamali (Habari Group), kimepatiwa msaada wa usafiri kwenda na kurudi mkoani Dodoma ili kujionea jinsi uendeshaji wa shughuli za Bunge unavyofanyika, anaripoti Rachel Balama
.Msaada huo wa usafiri umetolewa na Bunge wa Jimbo la Gairo,Ahmed Shabiby, ambapo mwaliko kwa kikundi hicho kwenda mkoani Dodoma umetolewa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki. Waziri huyo ndiye mlezi wa kikundi hicho.Wa k i w a mk o a n i h umo wanachama wa kikundi hicho watakuwa na mkutano na mlezi huyo pamoja na wadau
mbalimbali wakiwemo wabunge kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya kikundi.Akizungumzia udhamini huo, Shabiby alisema ameguswa na malengo ya kikundi hicho, na kuamua kukisaidia kama mchango wake kwa maendeleo ya taifa.Alisema, kwa kuwa kampuni yake ya usafirishaji abiria ni ya kizalendo na huwa anatoa misaada kwa makundi mbalimbali kama hayo kwa lengo la kuwakwamua kimaendeleo.
Mwenyekiti wa Habari Group, Mwanamkasi Jumbe, alimshukuru kwa udhamini huo, ambao unahusisha usafiri na kwamba inawapa moyo kuona viongozi na wafanyabiashara mbalimbali kuunga mkono juhudi za wasichana, hasa wenye malengo ya kujikomboa.
Alisema waandishi wa habari wengi wamekuwa hawana malengo, na mwisho wa siku kuishia pabaya, lakini wameamua kukusanya na kuweka akiba zao kwa manufaa ya baadaye.Alimsifu Angela, ambaye amekuwa akijitolea kwa kiasi kikubwa kuhakikisha kikundi hicho kinasonga mbele na kuomba wadau mbalimbali kujitokeza na kusaidia makundi kama hayo.  

No comments:

Post a Comment