- WAWILI WAOMBEWA ITC UJERUMANI
Na Mwandishi Wetu
KIUNGO wa Simba, Jonas Mkude ameitwa
kwenye kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la
Dunia dhidi ya Gambia
itakayochezwa Septemba 7, mwaka huu jijini Banjul.Kwa mujibu wa taarifa iliyolewa kwa
vyombo vya habari jana na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Boniface Wambura ilieleza kuwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen
amemuongeza mchezaji huyo ili kuimarisha sehemu ya kiungo.
Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager, imeingia kambini tangu Agosti 29 mwaka huu kwenye
Hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam.Wambura alisema timu hiyo imefanya
mazoezi jana asubuhi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume wakati leo saa 10
jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika hatua nyingine, Wambura alisema
Chama cha Mpira wa Miguu cha Ujerumani (DBU) kimetuma maombi ya Hati ya
Uhamisho wa Kimataifa (ITC), kwa wachezaji wawili wa Tanzania ili wajiunge na klabu
mbili tofauti za nchini humo.
Alisema maombi hayo yaliyotumwa kwa TFF
ni kwa ajili ya wachezaji Henry Claud Egito aliyezaliwa Desemba 31, 1984 jijini
Dar es Salaam, na Dominic Johnson aliyezaliwa Agosti 14, 1991 jijini Tanga.
Wambura alisema achezaji hao wanaombewa
ITC kama wachezaji wa ridhaa. Egito anaombewa
hati hiyo ili ajiunge na Klabu ya FSV Lokomotive Dresden wakati Johnson
anatakiwa na Klabu na TSV 1967 Schwabbruck
No comments:
Post a Comment