Na
Mwandishi Maalum
Rais Jakaya Kikwete, ametunukiwa Shahada
ya Uzamivu (PhD) ya Udaktari wa Sheria na Chuo Kikuu cha Guelph cha Toronto,
Canada, kutokana na mchango wake mkubwa wa kuleta mageuzi ya kilimo nchini na
Afrika kwa ujumla
. Rais Kikwete
alitunukiwa shahada hiyo juzi katika sherehe ya kufana iliyohudhuriwa na mamia
ya wasomi wa chuo hicho wakiwemo wanafunzi na wahadhiri na Wana-jumuya ya
Watanzania waishio Canada.
Rais Kikwete
ameitunuku Shahada hiyo kwa niaba ya wananchi wote wa Tanzania na hasa wakulima
wadogo ambao wanapigana kufa kupona kuboresha maisha yao kupitia kilimo. Hiyo ni heshima
ya juu kabisa ambayo Chuo Kikuu kinaweza kutoa; na Rais Kikwete anakuwa
Mtanzania wa kwanza kutunukiwa Shahada hiyo katika historia ya zaidi ya miaka
100 ya Chuo hicho, maarufu kwa utafiti wa kilimo na magonjwa ya wanyama.
Makamu Mkuu wa
chuo hicho na Kaimu Rais wa chuo hicho, Dkt. Maureen Mancuso, alifungua rasmi
Baraza la Kutunuku Shahada.
Akieleza sababu
ya kumtunuku shahada hiyo Rais Kikwete, Profesa Dkt. Kevin Hall, alisema chuo
hicho kimeamua kutoa Shahada hiyo kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza,
kuboresha na kuleta mageuzi katika kilimo cha Tanzania na Afrika.
“Tumeshuhudia
kwa namna isiyokuwa ya kawaida kabisa jinsi gani Rais Kikwete amekuwa sauti
isiyochoka ya kusemea kilimo cha Afrika na kuishawishi dunia katika kusaidia
kuleta mageuzi na mapinduzi ya kijani katika Bara hili muhimu sana kwa
kukabiliana na changamoto zinazokabili kilimo katika Bara la Afrika,” alisema
Dkt. Hall ambaye ni Makamu wa Rais wa Chuo hicho anayesimamia shughuli za
utafiti.
Aliongeza kuwa
kwa miongo mingi hawajashuhudia kiongozi mmoja wa Afrika akijitokeza kwa namna
isiyofichika kabisa kukabiliana na changamoto zinazokabili shughuli inayoajiri
watu wengi sana na ambayo ni tegemeo kubwa la maisha ya mamilioni ya watu.
“Rais Kikwete
tunakushukuru kwa mchango wako mkubwa katika kuleta mapinduzi ya kilimo katika
Afrika kupitia progamu zako kama vile Kilimo Kwanza na SACGOT,” alisema.
Rais Kikwete, kama kawaida yake
anapozungumzia shughuli za kilimo, ametoa hotuba ya kusisimua ambayo
ilizungumzia hali ya kilimo katika Tanzania na Afrika, changamoto kuu za kilimo
na hatua ambazo zinachukuliwa kukabiliana na hali hiyo.
Akizungumzia umuhimu wa kilimo katika
Tanzania, alisema kuwa asilimia 75 ya Watanzania wanaishi maeneo ya mashambani
na kutegemea kilimo kwa maisha yao na kuwa hata wale wanaoishi mijini uhai wao
unategemea kilimo kwa njia nyingi.
“Kilimo kinatupa chakula tunachokula,
mali ghafi ya viwanda vyetu, mapato yetu ya fedha za kigeni na ajira kwa ajili
ya watu wetu. Kilimo kinaingiza asilimia 25 ya Pato la Taifa, asilimia 34 ya
mapato yetu ya fedha za kigeni, asilimia 95 ya chakula chetu na kinaajiri
asilimia 75 ya watu wetu. Kwa ufupi basi, maendeleo ya uchumi na ustawi wetu
unategemea kilimo,” alisema.
Rais alisema pamoja na umuhimu huo wa
kilimo kwa Tanzania na Afrika, bado kilimo cha Bara hilo kinabakia cha jadi,
kilicho duni na chenye sifa ya uzalishaji mdogo.Niruhusuni nitoe takwimu kufafanua hoja
hii. Katika Tanzania hekta moja ya mahindi inazalisha tani 1.3, wastani wa
Afrika ni tani 1.9, katika China ni tani 5.7 na hapa Canada naambiwa ni tani
10. Vivyo hivyo, kwa uzalishaji wa mpunga na pamba.
Akizungumzia umuhimu wa kilimo katika
Tanzania, alisema kuwa asilimia 75 ya Watanzania wanaishi maeneo ya mashambani
na kutegemea kilimo kwa maisha yao na kuwa hata wale wanaoishi mijini uhai wao
unategemea kilimo kwa njia nyingi.
“Kilimo kinatupa chakula tunachokula,
malighafi ya viwanda vyetu, mapato yetu ya fedha za kigeni na ajira kwa ajili
ya watu wetu. Kilimo kinaingiza asilimia 25 ya Pato la Taifa, asilimia 34 ya
mapato yetu ya fedha za kigeni, asilimia 95 ya chakula chetu na kinaajiri
asilimia 75 ya watu wetu.
Kwa ufupi basi, maendeleo ya uchumi na ustawi wa wetu
unategemea kilimo,” alisema.Rais
alisema pamoja na umuhimu huo wa kilimo kwa Tanzania
na Afrika, bado kilimo cha Bara hilo
kinabakia cha jadi, kilicho duni na chenye sifa ya uzalishaji mdogo.
No comments:
Post a Comment