Na Mwandishi Wetu
Hali ya usalama
katika kambi ya wakimbizi Ndutta,si nzuri kutokana na ongezeko la vitendo vya
uhalifu vinavyofanywa na majambazi wanaofanya vitendo vya uhalifu nchunina
wenzao kutoka nchi jirani ya Burundi.
Kutokana na hali hiyo,Serikali ya Burundi
imeitaka Serikali ya Tanzania
kuendelea na msimamo wa kubadili matumizi ya ardhi katika kambi hiyo iliyopo
wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.
Akizingumza na Majira katika mahojiano maalum, Mkuu wa
Wilaya hiyo, Bw. Venance Mwamotto,alisema Serikali ya Burundi imefurahishwa na msimahuo kwani
majambaziwaliokuwa wakifanya uhalifu nchini kwao,walikuwa wakijificha eneo hilo.
“Kambi ya Nduta ipo mpakani mwa Tanzania
na Burundi,baada
ya wakimbizi waliokuwa wakiishi katika kambi hiyo kuondolewa, Serikali iliamua
kugawa ardhi kwa vijana ili kuwa na kijiji cha mfano katika swala la kilimo.” alisema.
Alisema awali Serikali ilitoa eneo hilo
kwa vijana amabao badala ya kuayatumia kwa kilimo cha mazao ambayo
yanayokubalika wao waliyatumia kwa kilimocha bangi,kuharibu mazingira na
wengine kuchoma miti ili kupata mkaa na kuuza.
“Ni hali ya kusikitisha,tumeweza kubaini tatizo hili
katika operesheni maalumtuliyoifanya katika eneo hili na kukamata kilo 1,500 za
bangi” alisema Bw. Mwamottto. Alisema uamuzi wa kubadili matumizi ya ardhi hiyo
ulifanywa na madiwani wa halmashauri hiyo na katika kikao cha maendeleo
wilayani humo ambapo kilibariki azimio hilo.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na mbunge wa Muhambwe,Felix Mkosamali
Aliongeza kuwa jambo la kushangaza Bw. Mkosamali watendaji
wenzake na kuamua kufungua kesi mahakamani na kudai vijana wameny’ang’anywa
ardhi. Bw. Mwamotto alisema kutokana na uhalifu uliokuwa ukifanyika eneo hilo umekuwa ulisababisha
hofu kwa wananchi..
Alisema hivi sasa ,uongozi wa Wilaya hiyo na
Jeshi la Polisi,umetangaza operesheni ya usalimishaji silaha,utoaji taarifa za
siri kwa watu wanaojihusihsa na matukio ya uhalifu
No comments:
Post a Comment