02 September 2013

ELIMU YA UFUGAJI YAANZA KUWAKOMBOA WAKULIMA



 Na Queen Lema, Arusha
ZAIDI ya wakulima 100,000 kutoka katika kanda mbalimbali nchini wamefanikiwa kupatiwa elimu ya ufugaji wa ng'ombe ili kuongeza uzalishaji wao ambao sasa umeongezeka kwa zaidi ya asilimia 80Wakulima hao walipatiwa elimu hiyo ya ufugaji wa ng'ombe na kuku kwa kipindi cha miaka miwili na Kampuni inayohusika na mifugo na mimea (KeenFeeders) iliyopo Jijini hapa.

Hayo yalisemwa jana na Ofisa Ugani wa Kampuni hiyo, Anzameni Muro, wakati akizungumza waandishi wa habari kuhusu hali ya Kilimo Kwanza hasa kwa Mkoa wa Arusha na Kanda ya Kaskazini kwa ujumla.
Muro alisema kuwa asilimia kubwa ya wakulima na wafugaji nchini bado wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa elimu ndiyo maana kampuni hiyo ikaanza kutoa elimu hiyo.
Alisema baada ya kuwapa elimu ambayo ilikuwa inahusu jinsi ya kupata faida kutokana na mifugo na mimea wameweza kuongeza uzalishaji wa maziwa na nyama kwa kiwango cha asilimia zaidi ya 80 tofauti na miaka iliyopita ambapo uzalishaji ulikuwa ni kama asilimia 20 hadi 40.
"Ukiwa kama mkulima au mfugaji ni lazima uweze kupata elimu, lakini hata vifaa ili kazi unayoifanya isiwe ni kazi ya mazoea tu, kama wadau wa Kilimo kwanza tuliweza kuliona hilo na tuliweza kuwapa elimu na kuwaelimisha hata namna ya kutumia virutubisho kama vile madini aina ya ng'ombe Mix,"aliongeza Muro.
Muro alisema kupitia elimu ya uhifadhi wa mazingira itaweza kuwasaidia wakulima wengi kwani mpaka sasa takwimu zinaonesha kuwa wapo wakulima ambao wanalima wakijua wanahifadhi mazingira, lakini kumbe
wanayahari

No comments:

Post a Comment