02 September 2013

AIRTEL YAPATA MKURUGENZI KITENGO CHA TEKNOLOJIA Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Airtel Tanzania imetangaza uteuzi wa, Frank Filman, kuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Teknolojia ya IT akichukua nafasi hiyo rasmi kuanzia sasaFilman ambaye ni mtanzania alianza kazi Airtel akiwa kama mwangalizi wa mifumo (System Admistrator) na baadaye alipanda cheo na kuwa Meneja wa Mradi wa Teknolojia ya IT. Kutoka mwaka 2007 mpaka 2009, alikuwa Meneja wa kitengo hicho nchini Ghana ambapo alisimamia na kutoa mchango mkubwa uzinduzi wa mtandao wa Airtel nchini Ghana.

  Mwishoni mwa mwaka 2009 Filman alirejea Tanzania akiwa kama Meneja wa Huduma za kimtandao za Airtel Tanzania.Baadaye alijiunga na kitengo cha mauzo na kama meneja wa Teknolojia na biashara ambapo aliweza kuchangia ongezeko la mapato kwa kiasi kikubwa hadi kufikia asilimia 100 kwa mienzi 12 tu.Katika miaka yake 12 na Airtel, Filman amefanya kazi miaka miwili, Airtel Ghana na zaidi ya miaka tisa akiwa na Airtel Tanzania.  
  Akizungumzia juu ya uteuzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso alisema "Uteuzi wa Filman kuwa Mkurugenzi wa kitengo cha Teknolojia ya IT ni ushahidi wa dhamira ya Airtel Tanzania kuendeleza, kulea na kukuza vipaji vya wafanyakazi wake ndani ya nchi.
"Sisi tunayo furaha kubwa kuona Watanzania wanachukua majukumu makubwa katika moja ya makampuni yanayokua kwa kasi na nyeti kama hii.Teknolojia ya IT ni msingi muhimu wa mafanikio katika mawasiliano ya simu kwa sababu huduma zetu mbalimbali ikiwa ni pamoja na huduma za kifedha yaani Airtel Money na internet zinategemea teknolojia hiyo."
Aliendelea kwa kusema Kampuni imemteua Bw. Filman ikiwa na uhakika kwamba ataifanya kazi hiyo kwa umakini mkubwa kabisa.Akizungumzia uteuzi wake Filman alisema, "Nimekuwa nikitamani kupata nafasi hii na nilijua siku moja naweza nikaipata na ninayofuraha kupata wadhifa huu Airtel Tanzania.
Kwa miaka mingi nimepitia mafunzo mbalimbali, na nina uzoefu nilioupata nchini Ghana pamoja na nchi nyingine Airtel inayofanya biashara. Hivyo niko tayari na nimejiandaa vyema kukabiliana na changamoto zote katika utendaji wa kazi hii na kuhakikisha natoa huduma zenye ubora kwa Watanzania  

No comments:

Post a Comment