03 September 2013

COCA-COLA YAZINDUA 'AMSHA MAISHA' KAMPUNI ya vinywaji b a r i d i y a Co c a -Co l a imezindua promosheni mpya ya 'Amsha Maisha Yako na Coca Cola' pamoja na wateja kujishindia pikipiki, anaripoti Mwandishi Wetu.Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo juzi meneja wa bidhaa wa Coca Cola Maurice Njowoka alisema wanunuzi wa bidhaa za kampuni hiyo watajipatia nafasi ya kushinda pikipiki 200.

 N j o w o k a a l i s e m a ma d h umu n i y a k u t o a pikipiki ni kusaidia kutoa ajira kwa vijana 200 ambao wataendesha ambapo kwa sasa zinatumika zaidi kwa usafiri wa haraka.“Tumeona ni vizuri kama safari hii tukatoa kitu, tungeweza kutoa magari, lakini yasingekua mengi kama hivi, tunaamini pikipiki ndiyo chombo kinachotumika zaidi kwa sasa,” alisema.
Al i s ema k i l a mt e j a atakayenunua vinywaji vya Coca Cola, Fanta, Sprite na Stone Tangawizi atapata nafasi ya kushinda pikipiki hizo kila kona ya nchi.“Kinachotakiwa kufanywa ni kukusanya vizibo vitatu vya soka ambapo ndani kutakuwa na alama tatu, moja kipande cha pikipiki cha mbele, kati na nyuma, hivyo ukipata vyote vitatu utakuwa umeshinda,” alisema.
Mbali na zawadi hiyo kutakuwa na pesa taslimu ambapo wanywaji wa soda watapata fursa ya kujishindia kuanzia sh. 1,500,000, 100,000, 50,000, 20,000, 10,000, 5,000 na soda ya bure.“Cha msingi kuzingatia ni kuwa kila kizibo chenye rangi ya dhahabu kitakuwa na zawadi,hakuna mambo ya jaribu tena, hivyo kila Mtanzania atakuwa na nafasi ya kushinda,” alisema.
Alisema promosheni hiyo itakuwa ni kwa nchi nzima na imeanza rasmi juzi, itaendelea mpaka Oktoba 30.
“Kama kampuni kila mwaka tunafanya kutoa asante kwa wateja wetu, mwaka jana tulikuwa na promosheni ya vuta mkwanja na watu wengi walinufaika, hivyo huu ni wakati wao kushinda pesa na pikipiki,” alisem

No comments:

Post a Comment