13 August 2013

PUSH MOBILE KUTOA VITZ 4 FIESTANa Namkeshe Ridhiwani
KAMPUNI ya Push Mobile Media Limited itatoa zawadi za magari manne aina ya Vitz na pikipiki 12 kwa mashabiki mbalimbali, watakaoshinda bahati nasibu maalumu ya tamasha la Serengeti Fiesta linalotarajiwa kuzinduliwa Jumamosi mjini Kigoma. Meneja Masoko na Mauzo wa Push Mobile Media, Rugambo Rodney alisema pia watatoa zawadi ya fedha taslimu sh. 100,000 kwa mashabiki hao.

Alisema ili kushinda wanatakiwa kutuma neno Fiesta kwenda namba 15678, ili kushinda gari, pikipiki au fedha na wanaweza kushinda tiketi ya VIP kwa kutuma jina la msanii kwa mfano Diamond na kuacha nafasi na baadaye kutuma maoni kwenda namba hiyo hiyo.Rodney alisema mbali ya kushinda tiketi, mshiriki atalipiwa tiketi ya ndege kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki katika tamasha la Fiesta la mwisho.
Alisema wameamua kuweka zawadi hizo, ili kunogesha zaidi tamasha hilo ambalo kwa kuwanufaisha mashabiki wa muziki hapa nchini.Aliongeza kuwa wamejipanga, ili kuwashirikisha wananchi wote katika tamasha hilo kwani pia watazindua huduma mpya ijulikanayo kwa jina la simu TV, ambapo itawawezesha mashabiki kuona video mbalimbali za muziki na matukio mengine, kupata nyimbo, kupata taarifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na za michezo kwa kupitia simu za mkononi.
Kuhusiana na zawadi za fedha, Rodney alisema zawadi hiyo itakuwa inatolewa kila siku kwa mashabiki watakaoshinda bahati nasibu hiyo.Alifafanua kuwa jumla ya sh. milioni

80 zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha shughuli hiyo itakayodumu kwa miezi mitatu.

No comments:

Post a Comment