16 August 2013

WIZARA MAMBO YA NJE YASHTAKIWA KWA SPIKA



Na Anneth Kagenda
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imesema Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imegoma kujenga majengo ya ubalozi nje ya nchi hivyo Serikali hulazimika kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kulipia kodi.

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Bw. Mussa Zungu, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema kutokana na hali hiyo, kamati hiyo imelazimika kuishtaki Wizara hiyo katika Ofisi ya Spika wa Bunge.
"Awali tuliiagiza Wizara hii ijenge majengo ya ubalozi nje ya nchi lakini inaonekana wamegoma kufanya hivyo... fedha nyingi zimepotea na zinaendelea kupotea kwa kuwapangia nyumba za mabalozi.
" T u m e p o t e z a p e s a isiyopungua sh. bilioni 130 kwa kipindi cha miaka 10 hadi sasa, wangekuwa wamejenga majengo yao tusingetumia fedha nyingi kulipia kodi," alisema.
Bw. Zungu alisema, hivi sasa wanasubiri mwongozo wa Ofisi ya Spika ambapo Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), lilishakubali kujenga majengo hayo lakini cha kushangaza Wizara husika bado imeendelea kuwakimy a.
Wa katihuo huo, kamati hiyoimemwagi za M kaguzi naMdh ibiti MkuuwaHesabuza Ser ikali (CAG) ,kufan ya ukaguziwathamani zaj engolaU kumbi waMwalimu Nye rere, ambalolilik abidhiwakwaWizara hiyo ikidai miundombinu yake ni mibovu.
Bw. Zungualis emakamatihiyoimeba iniviy oyozi vilivyopo katika jengo hilo havikidhi mahitaji, viti, vyoo na maji vyote viko katika viwango vya chini pamoja na kamati kutojua jengo hilo lilijengwa kwa gharama kiasi gani.
"Tumeambiwa Serikali ya China itatupa msaada wa kulipia asilimia 46.05 wakati Serikali ya Tanzania italipia asilimia 54 kwa mkopo usio na riba yoyote ambao utaanza kulipwa mwaka 2021 kwa kipindi cha miaka 10," alisema.

No comments:

Post a Comment