16 August 2013

SHULE 218 DAR HAZINA USAJILI



 Na Heri Shaaban
JIJI la Dar es Salaam lina shule za msingi na sekondari 218 ambazo zinaendelea kufundisha wanafunzi bila kuwa na usajili kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Katibu Tawala Mkoa huo Teresia Mbando, wakati wa kufunga kikao cha Umoja wa Walimu Wakuu wa Sekondari (TAHOSSA) Kanda ya Dar es Salaam.

Miongoni mwa shule hizo, za sekondari 59 na za msingi 159. "Tumezibaini shule hizi zinafundisha wanafunzi bila idhini ya Serikali na pia kuna vituo vya chekechea 1,029 havipo rasmi, vituo vya kufundisha masomo ya ziada 250 na hosteli 78," alisema na kuongeza;
"Vyote hivi ni bubu na ni changamoto kubwa kwa mkoa wetu kwani ndiyo chimbuko la watoto kufanya vibaya kwenye masomo yao." Alisema wenye vituo vya mitihani visivyo rasmi eneo la Mchikichini wana tabia ya kuongeza alama za masomo kwa wanafunzi ili kujipatia fedha kutoka kwa wazazi ili ionekane watoto wao wanaelewa wanachofundishwa.
Kwa u p a n d e wa k e Mwenyekiti wa TAHOSSA Kanda ya Dar es Salaam, Luteni Kanali Celestine Mwangasi, alisema mkutano huo ni wa pili kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.
Mwangasi alisema katika kikao hicho kinawakutanisha walimu wote wa shule za serikali na kawaida pamoja na wakaguzi wa shule na watu wa Baraza la Mitihani katika kujadili uandikishaji wanafunzi na usimamiaji mitihani na uendeshaji.
Ali s ema TAHOSSA Kanda ya Dar es Salaam ulianza mwaka 2009 ambapo changamoto kubwa katika sekta ya elimu ni ufaulu kwa wanafunzi ambapo umoja huo unaboresha mitihani ya ndani ili watoto waweze kufaulu katika ngazi ya taifa.  

No comments:

Post a Comment