Na Leah Daudi
SERIKALI imepiga
marufuku uingizaji, utengenezaji, uuzaji na utumiaji wa mifuko ya plastiki
nchini ikiwa ni jitihada za kuboresha usimamizi wa mazingira.Hayo yalisemwa na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dkt. Terezya Huvisa,
alipozungumza na waandishi wa bahari na kuongeza kuwa, watu wote ambao
watabainika kuzalisha au kuuza mifuko hiyo, watachukuliwa hatua.
Alisema Serikali
imechukua hatua hiyo ili kupunguza au kuondoa kabisa tatizo la kusambaa na
kutapakaa kwa taka za mifuko ya plastiki ambayo baada ya matumizi yake huishia
katika uchafu wa mazingira.
"Zuio hili
linahusu mifuko yote ya plastiki ya kubebea bidhaa kutoka madukani, sokoni na
majumbani isipokuwa mifuko yenye unene wa maikroni 100 inayooza na vifungashio
vya bidhaa mbalimbali kama vifaa vya hospitalini," alisema.
Aliongeza kuwa, agizo
hilo linapaswa kuzingatiwa na wenye viwanda, maduka na wananchi ili kutokomeza
kuenea kwa taka zinazotokana na mifuko ya plastiki kwenye mazingira.
Dkt. Huvisa alisema,
awali Serikali iliruhusu matumizi ya mifuko yenye unene usiopungua maikroni 30,
lakini kutokana na wananchi kutokuwa na uwezo wa kupambanua unene huo,
wafanyabiashara walitumia mwanya huo kuchanganya mifuko hiyo.
Alisema tatizo la
kuingia kinyemela kwa mifuko ya plastiki nchini linaongezeka kwa kasi hivyo ni
tatizo linaloikumba nchi zote za Afrika Mashariki.
" J i t i h a d
a z i n a h i t a j i k a k u h a k i k i s h a a g i z o h i l i
linazingatiwa, misako ya watu wanaofanya biashara ya mifuko hii itafanyika
maeneo yote ndani ya nchi na watakaokamatwa watachukuliwa hatua," alisema.
Alisema mswada wa
kupiga marufuku mifuko yote ya plastiki, uliwasilishwa katika Bunge la Afrika
Mashariki na kupitishwa na Bunge hilo Februari 3,2012.
Mswada huo uliridhiwa na marais wote wa nchi wanachama kwa lengo la
kupiga marufuku matumizi ya baadhi ya bidhaa za plastiki zinazochangia kuchafua
mazingira.
No comments:
Post a Comment