TAASISI za fedha
nchini zimeshauriwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa taasisi za elimu ili
ziweze kujipanua na kuchangia kuinua kiwango cha elimu nchini.Ushauri huo
ulitolewa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo,
Amos Makala, wakati akizungumza kwenye mahafali ya Shule ya Fountain Gate,
Tabata jijini Dar es Salaam, kukiwa na wahitimu 74 wakiwemo wa darasa la saba
na chekechea.
Alisema hakuna
haja kwa taasisi hizo kuogopa kuzikopesha taasisi za elimu kama Fountain Gate
kwani zina mali nyingi zisizo hamishika zinazoweza kutumika kama dhamana."Benki
zikiwakopesha wataweza kujipanua zaidi na Watanzania wengi watapata fursa ya
kusoma na katika elimu humo watapatikana akina Kikwete (Rais Jakaya Kikwete),
Pinda (Waziri Mkuu Mizengo Pinda) na wengine, nashauri taasisi za fedha ziwe
karinu na wadau wa elimu," alisema.
Awali, Mkurugenzi wa shule ya Fountain
Gate, Japhet Makau, alisema taasisi za fedha nchini zimekuwa na urasimu mkubwa
katika utoaji wa mikopo kwa taasisi za elimu hapa nchini.
Alisema taasisi za fedha zinapaswa
kuachana na urasimu huo na kuzipatia mikopo yenye masharti nafuu taasisi za
elimu ili ziendelee kutoa mchango mzuri katika kukuza elimu.
Makau alisema taasisi za fedha zinatakiwa
kuwa na mwenendo wa kibiashara wa taasisi za elimu na kubuni huduma
zinazoendana nazo.
Katika hatua nyingine, alisema shule hiyo
imeanzisha utaratibu wa kuwafadhili watoto yatima kusoma katika shule hiyo kila
mwaka ili wapate elimu bora kama wenzao wenye wazazi.
Alisema mwaka jana shule hiyo iliwafadhili
kwa asilimia 100 wanafunzi wawili kwa kuwalipia ada, mavazi, gharama za hosteli
na vifaa vingine vinavyohitajika.
"Fountain Gate tangu kuanzishwa kwake
imekuwa ikijali na kuwakumbuka watoto ambao wameshindwa kupata fursa ya elimu
baada ya kupoteza wazazi wao, familia ya shule hii wakiwemo wazazi, wafanyakazi
na wanafunzi wamekuwa wakiwasaidia nguo, vyakula na vifaa vya usafi,"
alisema.
Alisema Fountain Gate inajitahidi kutoa
elimu kamili kwa kutoa elimu kwa watoto wakiwa bado wadogo hadi chini ya miaka
miwili, kucheza, kujifunza kupitia michezo na kutoa msukumo wa kujifunza
kupitia ziara za mafunzo
No comments:
Post a Comment