Na Pendo Mtibuche, Dodoma
TANZANIA inakabiliwa na tatizo la watu
kutopenda bidhaa zinazozalishwa nchini na badala yake kukimbilia kuchangamkia
zile bidhaa zinazotoka nchi za nje.Hayo yalielezwa jana na Mkurugenzi wa Veta
Kanda ya Kati, Fredrick Mushi, wakati akizungumza na gazeti hili katika viwanja
vya Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nane Nene Nzuguni mjini hapa.
Kutokana na hali hiyo, mkurugenzi huyo
alisema VETA imekuwa mstari wa mbele kuwasogezea huduma wananchi na kuwapatia
elimu, hasa katika maonesho hayo ya wakulima ili waweze kuona ubora wa bidhaa
mbalimbali zinazozalishwa hapa nchini.
Al i s ema k uwa b i d h a a
zinazozalishwa nchini zikiwemo zile zinaozalishwa na VETA ni bora na hazina
madhara kwa mlaji au mtumiaji, hivyo Watanzania hawana sababu ya kukimbilia
bidhaa za nje na badala yake wajenge utamaduni wa kutumia bidhaa za ndani.
Hata hivyo, alisema kuwa bidhaa mbalimbali
ambazo wanazalisha ni zile zinazotokana na mbao, mazao ya chakula, mboga mboga
na zote hizo zinalenga kumuelimisha mkulima ili aweze kuona ni jinsi gani
watapenda bidhaa za ndani.
Akizungumzia maonesho hayo, alisema kuwa
VETA imejikita kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na mafunzo yanayotolewa katika
vyuo vyao vilivyopo kanda ya kati.
Alisema endapo bidhaa zinazozalishwa zinakuwa chini ya
kiwango walaji au watumiaji ndiyo wenye uamuzi wa mwisho wa kutozitumia bidhaa
za aina hiyo ili kutoa fursa kwa mtengenezaji aweze kuziboresha.
No comments:
Post a Comment