Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Vijana na
Michezo, Dkt. Fenella Mukangara jana alitangaza wajumbe watakaosimamia mbio za
Uhuru Marathon ambazo zinatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Desemba 8,
mwaka huu.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Dkt. Fenella alisema wajumbe wa
kamati hiyo itakayokuwa na watu 10 itakuwa na jukumu la kuhakikisha mbio hizo
zinafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Kamati hiyo
inatarajiwa kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq huku
ikiwa na wajumbe wengine kutoka katika sekta mbalimbali nchini.
Wajumbe wengine
katika kamati hiyo iliyoundwa na Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia
Mjema, Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, Naibu Mkurugenzi
wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana
Yassoda na Mkurugenzi msaidizi Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa.
Wengine ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Intellectuals, Innocent Melleck, Kaimu Mhariri
Mtendaji wa magazeti ya Serikali (TSN), Gabriel Nderumaki, George Kavishe
kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mhariri Mtendaji wa Uhuru, Jossiah Mfungo
na Habib Gunze wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
Waziri Fenella
alisema mbio hizo zitakuwa zimegawanyika katika sehemu nne kukiwa na mbio ndefu
za kilomita 42, mbio za kati kilomita 21, mbio za kujifurahisha kilomita 5 na
mbio fupi ambazo ni maalumu kwa viongozi zikiwa za kilomita 3.
"Mbio hizi zina lengo kuu la
kuimarisha umoja, upendo, mshikamano na amani kwa Taifa letu. Tunategemea
Watanzania wengi, ikiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini,
wanafunzi wa ngazi mbalimbali na wananchi kwa ujumla wataungana na kushiriki
mbio hizi," alisema.
Naye Mratibu wa Uhuru Marathon,
Innocent Melleck alisema wazo kubwa la kuanzisha mbio hizo ilikuwa ni kutaka
kuwakumbusha Watanzania k u u e n z i umo j a , ama n i , mshikamano ulipo
pamoja na uhuru wetu.
Mratibu huyo alisema, mpaka sasa
wanariadha zaidi ya 300 kutoka nje ya Tanzania wameomba kushiriki mbio hizo za
aina yake hapa nchini.
"Sisi kama vijana tukaona kuna
haja ya kufanya kitu cha kuwakumbusha Watanzania wenzetu kwani tunatakiwa
kudumisha urithi wa amani, mshikamano na uhuru wetu tulioachiwa na mababu
zetu," alisema.
Melleck alisema mbali na mbio hizo
kufanyika siku hiyo, pia kutakuwa na tamasha kubwa la burudani litakalofanyika
katika Viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni, Dar es Salaam ikiwa ni mkesha
wa kusubiri siku ya Uhuru.
Mbali na hayo Waziri Fenella
naye alizitaka taasisi mbalimbali kuhakikisha wanazidhamini mbio hizo kwani
zina manufaa makubwa kwa taifa.
No comments:
Post a Comment