27 August 2013

WAZEE 300 WAUAWA KILA MWAKA



 Na Theonestina Juma, Kagera
ZAIDI ya wazee 300 huuawa hapa nchini kila mwaka kutokana na umaskini na uchu wa kutaka mali na si kwa madai ya ushirikina kama inavyodaiwa katika jamii. Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mratibu wa chama cha Saidiawazee wilayani Karagwe (SAWAKA), Livingstone Byekwaso katika warsha ya siku moja iliyoendeshwa na chama hicho kwa waandishi wa habari mkoani Kagera kuwajengea uelewa juu ya ufuatiliaji wa matatizo yanayowakabili wazee.

Alisema, "kila mwaka wazee zaidi ya 300 wanauawa hapa nchini kwa tuhuma za uchawi si kweli, tatizo kubwa ni kunyang'anywa mali zao; na hii inatokana na umaskini uliopo kwa baadhi ya vijana na ukosefu wa ajira," alisema.
Alisema wazee hao zaidi ya 300 wamekuwa wakiuawa hasa Kanda ya Ziwa, katika Mikoa ya Kagera, Simiyu, Shinyanga, Geita, Mwanza na Tabora. Pia wazee hao wamekuwa wakinyanyaswa zaidi katika Mkoa wa Kagera ambapo wazee wamekuwa wakifyekewa mashamba yao.
Alisema wazee wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo maagizo yanayotolewa na Serikali hayapewi uzito wowote kama ya kutibiwa bure katika hospitali za umma.
Alisema wazee wamekuwa wakitwikwa mzigo wa kulea watoto yatima ambao wazazi wao hufariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ukimwi.
Alisema asilimia 54 sawa na watoto yatima milioni mbili wamekuwa wakihudumiwa na wazee baada ya wazazi wao kufariki kwa ugonjwa wa Ukimwi.
Halikadhalika alisema, asilimia nne ya wazee hapa nchini ndiyo wako katika mfumo wa pensheni na asilimi 96 wanaobaki hawamo katika mfumo huo jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa kuishi katika mazingira magumu ikiwemo namna ya kupata mahitaji yao ya kila siku kama chakula, malazi na mavazi.
Naye Makamu Mwenyekiti wa umoja wa Shirika la Tanzania Social Protect Network, Ramadhani Msoka katika ripoti ya Shirika la Haki za Binadamu mwaka 2011

No comments:

Post a Comment