Na Penina Malundo
WA Z A Z I n a w a l e z i n c h i n i w ame s h a u r i w a
kufuatilia kikamilifu maendeleo ya kitaaluma ya watoto ili kupunguza ongezeko
la matokeo mabaya ya mitihani yao
ya mwisho.Ushauri huo
ulitolewa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na
Mkuu wa Jimbo la Kati la Dayosisi ya Mashariki (KKKT), Chediel Lwiza wakati wa
mahafali ya tatu ya wahitimu wa Shule ya Msingi ya Mount Zion iliyopo jijini humo
. Lwiza alisema
kuwa kutokana na wimbi kubwa la ongezeko la wanafunzi wanaofeli kidato cha pili
na nne ,ipo haja ya wazazi na walezi kushirikiana na walimu, kuhahikisha
wanaimarisha misingi ya elimu kuanzia nyumbani wanapotoka watoto hadi wafikapo
shuleni.
"Elimu bora
inatokana na ushirikiano mzuri baina ya mwalimu na mzazi na hapo mzazi unauwezo
wa kupokea matokeo mazuri kutoka kwa mtoto kwani jukumu la kusimamia kama mtoto
anasoma si la mwalimu peke yake bali hata mzazi anawajibu wa kusimamia mwenendo
wa masomo ya mtoto wake hasa kipindi mtoto yupo nyumbani," alisema Lwiza
Alisema asilimia
kubwa ya jamii inayowekeza katika elimu inauwezo mkubwa wa kutengeneza Taifa
lenye maendeleo na lenye kuleta misingi imara itakayoweza kuleta tija ya kuinua
nchi katika nyanja ya uchumi, kijamii na kisiasa.
Aidha alisema
kuwa shule za msingi pamoja na sekondari zinatakiwa kuwafundisha wanafunzi kwa
njia ya vitendo zaidi hasa somo la ujasiriamali kama somo la ziada
litakalomuwezesha mwanafunzi pindi atakapo maliza shule na kukosa ajira kuweza
kujiajiri mwenyewe.
"Hakuna mtoto hata mmoja
anayezaliwa akawa mbumbumbu, ila Mungu kila mtu kampatia uwezo wake hivyo
nashangazwa na Wazazi wanaokata tamaa dhidi ya watoto wanaofeli mitihani kwani
mungu anajua kuwa kila mtu anauwezo wa kufanya jambo fulani, hivyo ni vyema
tukawekeza watoto wetu elimu iliyobora nakuimarisha misingi imara ya elimu
itakayomfanya watoto waondokane na kufeli," alisema.
Jumla ya wanafunzi 29 wa Shule
ya Msingi Mount Zion waliomaliza darasa la saba na awali, wamekabidhiwa vyeti
vyao katika mahafali hayo.
No comments:
Post a Comment