WATU wenye matatizo
na maradhi ya moyo wametakiwa kutotumia kinywaji kipya cha Chilly Willy ili
kujiepusha na usumbufu ambao ungeweza kuwapata kama
wangetumia kinywaji hicho pasipo kujua madhara yake, anaripoti Mwandishi
Wetu.
Ushauri huo
umetolewa na Meneja Uhusiano wa Super Market ya TSN, Meshack Nzowah, wakati wa
promosheni ya kinywaji hicho iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
katika hafla hiyo Nzowah alisema Chilly Willy ni kinywaji kisicho na kilevi
kinatumika kwa watu mbalimbali na kinaongeza nguvu kwa watumiaji, lakini kwa
watu wenye matatizo ya moyo hakiwafai.
Aliongeza kuwa
kinywaji hicho kinachotengenezwa Dubai,
kinapendwa na watu mbalimbali duniani hususan wanamichezo na kimekuwa
kikiwaongezea nguvu.
“Baada ya kuona
kinywaji cha Chilly Willy kinatumiwa na watu wengi duniani, tumeamua kukileta Tanzania ili
watu waanze kukitumia kwa kweli ni kinywaji bora na kinakata uchovu wa
pombe,”alisema Nzowah.
Watu wengine
ambao hawatakiwi kutumia kinywaji hicho ni watoto walio chini ya miaka 10.
Aliwataka Watanzania waanze kutumia kinywaji hicho.
Licha
ya uzinduzi huo kufanyika jijini Dar es Salaam, pia uzinduzi kama hao
ulifanyika visiwani Zanzibar
ambapo wananchi mbalimbali wameshauriwa kutumia kinywaji hicho.
No comments:
Post a Comment