Na
Hamisi Nasiri, Masasi
MBUNGE wa Jimbo
la Masasi (CCM)mkoani Mtwara, Mariam Kasembe amewataka watendaji katika
Halmashauri ya mji wa Masasi kuwa wabunifu katika suala la mipango miji ili
kuufanya mji huo uwe katika mandhari ya kuvutia hatimaye kuondokana na tatizo
la ujenzi holela.
Mbunge huyo aliyasema hayo mwishoni mwa wiki kwenye kikao cha kawaida
cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya mji wa Masasi wakati alipokuwa akitoa
nasaha kwa madiwani na watendaji wa Halmashauri hiyo, baraza hilo lilifanyika
katika ukumbi wa nje wa karakana ya maji mjini hapa.
Alisema kuwa watendaji waliopo kwenye Halmashauri hiyo ni lazima wawe
wabunifu katika kuhakikisha kuwa mji huo unakuwa safi na kuhakikisha kuwa
wananchi wanajenga majengo yao kuendana na kanuni na taratibu za mipango mji
zinavyotaka ili mandhari ya mji iwe katika hali inayotakiwa.
Kasembe alisema kuwepo kwa tatizo la mipango mji katika mji wa Masasi
linaweza kwisha iwapo kila mtendaji kwa nafasi yake atakuwa mbunifu katika
kutimiza wajibu anaotakiwa kuufanya hatimaye mji kuwa kwenye mwonekano
unaotakiwa na hata ubunifu huo pia utasaidia kuleta maendeleo mengine kwa
wananchi.
Alisema kuwa msingi wa mji kuwa katika mandhari inayotakiwa kutokana na
watendaji husika kuwa wabunifu kwenye kubuni na kusimamia mipango mbalimbali ya
kuuweka mji kwenye ramani mzuri ya kuvutia na kufanya tatizo la makazi holela
kutoweka.
Ai d h a mb u n g e h u y o a l iwa s h a u r i wa t e n d a j i
waliyopo kwenye Halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa wanatekeleza ipasavyo
mahitaji yanayowagusa wananchi ili kupunguza malalamiko yasiyo na msingi
ikiwemo malalamiko ya viwanja ambapo katika eneo la kata ya Nyasa na Mtandi
baadhi ya wananchi wamelipia zoezi la upimaji lakini hadi sasa upimaji
haujafanyika.
"Nawaomba watendaji kuweni
wabunifu ili mji wetu uwe katika mandhari ya kuvutia kwa wageni wanaoingia na
kutoka lakini kama msipokuwa na ubunifu mji utaendelea kuwa katika hali mbaya
...pia naomba kila mtendaji kupitia nafasi yake pia awe mbunifu ili kwa pamoja
tuweze kuwatimizia wananchi kile wanachokihitaji," alisema mbunge huyo.
No comments:
Post a Comment