05 August 2013

MSHINDI WA NYUMBA PROMOSHENI YA AIRTEL YATOSHA KUPATIKANA LEO


Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya simu ya Airtel itachezesha droo ya kwanza ya mwenzi ya promosheni ya Shinda Nyumba na Airtel Yatosha leo ili kumtafuta mshindi wa nyumba ya kisasa iliyoko Kigamboni jijini Dar es Salaam
.Akizungumza kuhusu droo hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando, alisema Airtel kupitia promosheni ya Airtel yatosha inaendelea kuwazawadia wateja zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu kiasi cha sh. milioni moja kila siku.
Aliongeza kuwa zaidi ya wateja 21 wamejishindia kiasi cha zaidi ya sh. milioni 21 na bado kuna nafasi kwa wateja zaidi ya 69 kuondoka na kitita cha kiasi hicho kila siku.
Meneja huyo aliendelea kusema kuwa mbali na zawadi ya sh. milioni moja, Airtel pia inatoa zawadi ya kila mwezi kwa mshindi ambapo nyumba tatu za kisasa zimejengwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC maeneo ya Kigambopni jijini Dar es Salaam.
"Natoa mwito kwa wateja ambao bado hawajajiunga huduma ya Airtel yatosha kujiunga kwa kununua kifurushi cha wiki, siku au mwezi na kuunganishwa moja kwa moja kwenye promosheni na kupata nafasi ya kuingia kwenye droo ya kuibuka mshindi wa nyumba au fedha kila siku," alisema Jackson.
Kwa upande wake Ofisa Habari wa Shirka la Nyumba la NHC, Yahaya Charahani, alisema nyumba zimekamilika na zipo tayari kukabidhiwa kwa washindi. "Tunaamini mshindi atakayepatikana atafurahia mandhari mazuri, mazingira na nyumba yenye ubora wa kiwango cha juu.
Nachukua nafasi hii kuwahimiza Watanzania wapate muda wa kutembelea nyumba hizi ili nao wapate nafasi ya kuona miradi mbalimbali tuliyonayo," alisema

No comments:

Post a Comment