Na Steven William, Muheza
WANANCHI wa Kijiji cha Kwelumbizi Kata
ya Zirai Tarafa ya Amani wilayani Muheza wameiomba Serikali kuzishawishi
kampuni za simu za mkononi kujenga minara katika kijiji hicho cha Kwelumbizi
ili wananchi wapate mawasiliano ya uhakika kwani kwa sasa wanapata shida.
Wananchi hao
walisema kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakipata tabu ya mawasiliano kutokana na
kutokuwepo minara ya mawasiliano hivyo kuzidi kuwarudisha nyuma katika harakati
za maendeleo.
Mmoja wa wakazi
wa kijiji hicho, Tekra Jemes Makundi alisema kuwa kwa sasa wakitaka kuwasiliana
na watu huko mjini mpaka wapande juu ya miti mirefu ndiyo wanapata mawasiliano
kupitia mnara kutoka Maramba wilayani Mkinga.
Alisema kuwa
kutokana na hilo tayari baadhi ya watu wameshaanguka na kuvunja miguu kwa ajili
ya kutafuta mawasiliano juu ya miti, Makundi ambaye ni mfanyabiashara wa
kukusanya iliki na mdalasini alisema kuwa wanamuomba Waziri wa Mawasiliano
kuzishawishi kampuni za simu kujenga mnara katika kijiji hicho kwa kuwa kina watu
wengi wanaomiliki simu na kinawafanyabiashara wengi.
Nae Mwenyekiti wa Kijiji cha
Kwelumbizi, Shabani Kipala alisema kuwa wameweza kuleta maendeleo ndani ya
kijiji hicho kwa kujenga shule ya sekondari ya kata ya Zirai na kuomba serikali
kuongeza walimu shuleni hapo
No comments:
Post a Comment