13 August 2013

WANYARWANDA 2000 WAREJEA MAKWAO



Na Livinus Feruzi, Bukoba
WAHAMIAJI haramu zaidi ya 2,000 wameondoka mkoani Kagera na kurudi kwao nchini Rwanda
tangu Rais Jakaya Kikwete, atoe siku 14 kwa wahamiaji kuondoka nchini kwa hiari ndani ya kipindi hicho.
Rais Kikwete alitoa agizo hilo akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Kagera, ambapo agizo hilo lilihusu mkoa huo pamoja na Geita na Kigoma. Mbali na wahamiaji haramu, Rais Kikwete aliwataka watu wanaomiliki silaha kujisalimisha kwa hiari yao kabla ya msako mkali kuanza. Takwimu za kuondoka kwa wahamiaji haramuzaidi ya 2,000 mkoani Kagera, zilitolewa na Mkuu wa Mkoa huo, Kanali Mstaafu, FabianiMassawe, wakati akizungumzia maandalizi ya kuanza operesheni ya kuwaondoa kwa nguvu baada ya kumalizika kwa siku 14 alizotoa Rais Kikwete. Massawe alisema hadi sasa taarifa ambazo wamekusanya kuhusiana na wahamiaji haramu wanaondoka kwa hiari yao kwa upande wa Rwanda wamefi kia zaidi ya watu 2,000.Hata hivyo alisema takwimu kutoka nchi nyingine bado hazijafahamika kutokana na wahamiaji hao kupita njia za mkato.”
Wahamiaji wa nchi nyingine hazijapatikana lakini wameondoka kwa kiasi chake kupitia njia
za panya,” alisema. Katika hatua nyingine, Massawe alisema operesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu
itaanza wakati wowote kuanzia leo, baada ya kumalizika kwa siku 14 zilizotolewa na rais. Aliwataka wananchi mkoani Kagera kutoa ushirikiano wakati wa operesheni kwa kuwafi chua wahamiaji haramu na watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria. Alisema ushirikiano wa wananchi ndio utakaosaidia kufanikisha operesheni hiyo ambayo itangazwa na Rais Kikwete katika mikoa mitatu ambayo ni Kagera, Geita na Kigoma.
“Operesheni iko pale pale na muda wowote itaanza, baada ya muda waliopewa kukamilika, hivyo ndugu zangu wananchi wa Mkoa wa Kagera tuwe wazalendo kuwafi chua wahamiaji haramu,” alisema. Alifafanua kuwa watakaokamatwa wakati wa operesheni hiyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani. Aliwaomba wananchi wa Mkoa wa Kagera kutoa taarifa za wahamiaji haramu na watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria ambao zinaweza kusababisha madhara kubwa miongoni
mwananchi na taifa kwa ujumla

2 comments:

  1. Je mikoa mitatu tu ndiyo inao wahamiaji haramu?tu.pia kwanini msako huwa haupiti katika viongozi wa serikali?mimi ninaamini kuna wahamiaji wengi wanafanya kazi katika idara mbalimbali za kiserikali na kijamii lakini kwakuwa wamehifadhiwa na wakubwa hawatolewi nje.tatu je ni mfumo gani nchi yetu ya tanzania tunao.kulingana wapo watoto waliozaliwa hapo tanzania hawajuhi nchi nyingine yoyote iwapo wazazi wao wametoka nchi za nje je hao watoto kwanini wanahitwa ni wahamiaji haramu na huku wakiwa wamezaliwa tanzania je hiyo ni haki?pia je hivyo ndivyo katiba ya nchi inavyosema?naomba serikali mchunguze mambo kama hayo kabla ya msako wenu huo.Nne wakati vyombo vya sheria vinaposema vitashirikiana na raia kwa kuwatoa wahamiaji haramu je haoni hapo haki haitatendeka?swali la mwisho je wale wanyarwanda ,wakongomani ,warundi waliokuja tanzania tangu miaka ya 1960.1964,1972.wameishi hapo tanzania miaka yote hii je itakuwaje leo hii muwaambie kwamba waende makwao?huku wakiwa na watoto katika idara mbali mbali.mfano jeshi,mahakami,hospitalini, police,ikulu,bungeni na idara nyingine mbalimbali.je hawa wazee wataacha watoto wao.swali la mwisho kuna wazazi waliotoka nchi za nje wakakimbilia hapo tanzania lakini kwa bahati mbaya wameshafariki.lakini waliacha watoto hapo tanzania na hao watoto hwajuwi wapi wazazi wao walikotokea je hao watoto mtawapeleka wapi msako ukianza.ushauri nawaombeni viongozi mtakao fanya msako muwe makini sana kwa kuzingatia haki.

    ReplyDelete
  2. Jamani Serikali isafishe hadi Ukerewe mkoani Mwanza, wamejaa Warundi na Wahutu wa Rwanda kibao kwani lugha inafanana na si rahisi kuwagundua.

    Vitambulisho vingekuwepo ingefaa. Wanaua watu usiku na mchana, kwenye vinjia na ziwani.

    Wanajifanya ni Wakerewe, au Wajita au Wakara, kumbe ni watu wa NBurundi na Rwanda, jamani Serikali iko wapi jamani eeh??

    Pia huko Karagwe, Ngara ,a Biharamulo, wamejaa sana.
    Ukienda kwenye visiwa vidogo vidogo ziwani Victoria wamejaa, visiwa vidigo mno vinajulikana kama VIZINGANI. Mtu hakatishi, anakua.

    Watoeni watu hawa warudi kwao Rwanda. Hata Waruhdi watoeni wanaua watu sana.

    Wamiliki wakubwa wa Bunduki na Bastola ni Warundi na Wahutu wa Rwanda. Wana mifugo kibao, wamengia sasa Kigoma vijijini hko wako kibao, Serikali inaruhusu tu. Wenyeviti wa Vijiji huko Karagwe, Ngara, Kigoma na Biharamulo, wengi wao ni wahamiaji wa miaka karibu 100 hivyo bado wana damu ya kwao na wanawalinda wahamiaji toka kwao wanapo ingia hapa Tanzania kupitia njia za uchochoroni na vichakani au kupitia Mitoni. Polisi wapelekwe kwenye njia hizo za panya.

    Mwanza pia wako kibao warundi na wanyarwanda kule makorobo na kwenye mitumba kote ni wao, lugha yao kama Kizanani, si rahisi kuwatambua, wanajichanganya wanaongea kiswahili safi. Uchunguzi wa hali ya juu unahitajika.

    ReplyDelete