07 August 2013

WANAUME 100,000 KUFANYIWA TOHARA


Na Derick Milton, Simiyu
ZA I D I y a w a n a ume 100,000 katika Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, wanatarajiwa kufanyiwa huduma ya tohara ndani ya miaka mitano.Hatua hiyo inaenda sambamba na utekelezaji wa mradi wa tohara kwa wanaume wilayani humo ulioko chini ya shirika lisilo la kiserikali la Intra Health kwa kushirikiana na Serikali.

Mradi huo ambao uko chini ya shirika hilo linalojishughulisha na utoaji huduma za afya kwa jamii unalenga kuwafikia jumla ya wanaume 127,840, kwa kipindi cha miaka mitano ambapo idadi hiyo ya wanaume ni kuanzia umri wa miaka 10 hadi 30.Hayo yalibainishwa jana na Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Dkt. Assey John katika ufunguzi wa kituo cha kutolea huduma hiyo katika Hospitali ya wilaya, ufunguzi uliofanywa na Mwenge wa Uhuru unaokimbizwa katika wilaya hiyo.
Dkt. Assey alisema kuwa mradi huo ulianza mwaka 2010 ambapo mpaka sasa una miaka mitatu tangu uanzishwe na unatarajiwa kufikia mwisho wake mwaka 2015 ukiwa umefikisha miaka mitano.Aliongeza kuwa, katika ujenzi wa kituo hicho kiasi cha sh. milioni 58.4 huku lengo likiwa ni kupunguza maambukizo ya Virusi vya Ukimwi kwa asilimia 60.
Alibainisha kuwa, tangu kuanzishwa kwa mradi huo jumla ya wanaume 27,969 kutoka mwaka 2010 hadi Julai mwaka huu wameshapatiwa huduma hiyo.Mbali na hayo alibainisha kuwa, mradi huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo ni kukosekana kwa elimu kwa wanaume juu ya umuhimu wa huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment