07 August 2013

MAUAJI YA ALBINO YAITIA DOA NCHI


Na Grace Ndossa
SERIKALI imesema kuwa imekosolewa kuhusiana na mauaji ya albino katika Mpango wa Kujitathmini Kiutawala Bora Afrika (APRM) na kutakiwa kujirekebisha ili yasitokee tena.Hayo yamesemwa juzi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, George Mkuchika katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa televisheni ya ITV
.Alisema kuwa kwa nchi wanachama wa APRM wa l i o n a n i j amb o l a ajabu kumuua binadamu mwenzako kwa imani ya kupata utajiri."Ni J amb o l a a i b u ambalo nchi wanachama wanashangazwa kuwepo kwa mauaji ya albino ili kupata utajiri kwani wanachama hao wamedai wao hawajawahi k u o n a mt u a n amu u a binadamu mwenzake kwa imani ya kupata utajiri," alisema Mkuchika.
Alisema kuwa kutokana na changamoto walizopewa wameahidi kuzifanyika kazi ili kuondoa aibu hiyo kwa nchi.Kwa upande wa rushwa alisema kuwa Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi kumi kati ya nchi wanachama 54 ambazo zinapambana na wala rushwa.
Alisema kuwa tatizo la rushwa ni pana na wanaendelea kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuhakikisha wanadhibiti hali hiyo.Alisema kuwa hakuna watu wanaoshindwa kupambana na papa na nyangumi tatizo ni vitendea kazi pamoja na uhaba wa fedha katika ofisi za TAKUKURU ili kuwawezesha wakaguzi kufanya kazi nchini na nje ya nchi kutokana na ufinyu wa bajeti.
Hata hivyo alisema kuwa wananchi wanatakiwa kushirikina na vyombo vya dola katika kuhakikisha wala rushwa wanafichuliwa.
.

No comments:

Post a Comment