Na Esther Macha, Mbeya
WANANCHI wa Kata ya Mshewe Kijiji cha
Njelenje Wilaya ya Mbeya wamelalamikia kukosekana kwa maji kwa muda wa miaka 10
licha ya uongozi wa kata hiyo kuendelea kuwachangisha michango ya mabomba
wananchi hao
Walisema ni
jambo la kusikitisha kuona uongozi uliopo unafanya kazi ya kuchangisha michango
tangu mwaka 2009 mpaka sasa na dalili za kuwepo maji hakuna na hata kusomewa
mapato na matumizi ya fedha hizo hayapo.
Uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)
umebaini kuwa maji ambayo wanatumia wananchi wa kijiji hicho ni yale ambayo
yanatoka kwenye chanzo ambacho ni makaburi ya watu ambayo hata hivvyo hayana
usalama wowote ambapo gazeti hili lilibaini kuwa maji hayo ambayo yapo kwenye
chemchem.
Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha
Njelenje, Rashid Odati alisema kuwa toka wameanza kuchangia maji ni muda mrefu,
kwani maji yaliyopo ambayo wanatumia ni hatari kwa afya za wananchi kutokana na
maji wanayotumia kutoka kwenye chanzo ambacho kipo karibu na vyoo na makaburi
ya watu.
"Hapa tulipo hatuelewi hatma yetu
ni nini kwani maji tunayotumia ni hatari sana kwa afya zetu hebu ndugu
mwandishi wa habari angalia hicho chanzo kipo kati kati ya makaburi kwa hali
hii sidhani kama kuna uhakika wa sisi wananchi kupata maradhi," alisema
mkazi huyo.
Akizungumzia kuhusu viongozi alisema
wamekuwa na sababu nyingi za kutoa kwa wananchi ambazo hazina umuhimu wowote
kutoka kwa wananchi kwani fedha ambazo zinachangwa na zimekuwa kama mtaji kwao
wa kuendeshea maisha yao.
"Mfano huyu diwani wetu† amekuwa
na amri zake kwa wananchi kwa kutumia cheo chake kukandamiza wananchi , sisi
hatutaki diwani awe mwiba kwetu kwa kutumia† nafasi yake kama fimbo kwa
wananchi," alisema Odati.
Mkazi mwingine, Teddy Mwakaje alisema
kutokana na shida ya maji hakuna maendeleo yeyote ambayo wanafanya kutokana na
muda mwingi kutumia kutafuta maji kwani hata yaliyopo kwenye chazo nayoi bado
ni tatizo kuyapata licha ya kutokuwa na usalama wa kutosha.
Akizungumzia tatizo hilo la maji
Mwenyekiti wa kitongoji cha Kizota, John Kapange alisema kuwa kero hiyo ya maji
ni ya muda mrefu katika kijiji hicho na kusababisha wananchi kutoka usiku wa
manane kwenda kutafuta maji kwenye visima.
Akijibu
malalamiko hayo ya wananchi Diwani wa Kata ya Mshewe, Fabian Mwakasole alisema
tatizo hilo la maji katika Kijiji cha Njelenje ni la muda mrefu na kwamba toka
anaingia madarakani mwaka 2010 amelikuta.
No comments:
Post a Comment