Na Florah Temba, Moshi
KATIKA
hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya wananchi mk o a n i Ki l ima n j a r o ,
wamelazimika kutumia mifuko ya plastiki (malboro) kujikinga na maambukizo ya
ugonjwa wa Ukimwi, huku wengine wakichangia kondomu, jambo ambalo ni hatari na
linaelezewa kuwa moja ya chanzo cha ongezeko la maambukizo mapya ya ugonjwa huo
mkoani humo
. Takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha maambukizo ya
ugonjwa wa Ukimwikatika Mkoa wa Kilimanjaro, kimepanda kutoka asilimia 1.9
mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 3.8 mwaka 2011/2012.
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake, Mkurugenzi
Mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali, linalojihusisha na mapambano
dhidi ya Ukimwimkoani Kilimanjaro (KACA) Faraji Swai alisema wananchi wa maeneo
ya vijijini wako hatarini zaidi kupata maambukizo ya ugonjwa ya ukimwikutokana
na kwamba wengi bado hawajafikiwa.
Alisema Shirika la Kacakatika utoaji elimu ya mapambano
dhidi ya Ukimwikwa jamii, wamefika katika baadhi ya vijiji mkoani Kilimanjaro
na kuwakuta wananchi wakitumia mifuko ya plastiki (malboro) kama kinga ya
kujikinga na maambukizo ya Ukimwihuku wengine wakichangia kondomu jambo ambalo
liliwashangaza.
Alisema vijiji ambavyo walikuta wananchi wakitumia
malboro kujikinga na Ukimwina kuchangia kondomu ni pamoja na Kahe, Mikocheni, Newland
na TPC vyote vya Wilaya ya Moshi, huku baadhi ya mitaa katika Kata ya Njoro
Manispaa ya Moshi wakikutwa nao wakichangia kondomu moja zaidi ya mtu mmoja.
"Ni jambo la kushangaza kwani yapo maeneo katika Mkoa huu wa
Kilimanjaro ambayo tumefika kutoa elimu ya kujikinga na maambukizo ya Ukimwina
wananchi kutueleza kuwa wao hutumia malboro kama kondomu kujikinga na ugonjwa
huo huku wengine wakifua kondomu mara baada ya kutumia ili kutumia tena wakati
mwingine au kumpa mwenzake naye ajikinge, kwa kweli hii ni hatari sana,"
alisema Swai.
Alisema maeneo ya mjini kondomu zimekuwa zikizagaa kwa kukosa watumiaji
lakini yapo maeneo ya vijijini yenye uhitaji mkubwa na hayajafikiwa jambo
ambalo limesababisha kasi ya ukimwikatika maeneo hayo kuzidi kukua.
Alisema maeneo mengine ambayo yameonekana kuwa na kasi ya maambukizo ya
Ukimwina yanauhitaji mkubwa wa kondomu ni Kibosho, Mwika na Marangu Mtoni hivyo
kunahitajika jitihada za makusudi za kuwanusuru wananchi wa maeneo hayo.
Swai aliongeza kuwa zipo sababu nyingi ambazo zinachangia kasi ya
maambukizo mapya ya Ukimwiambapo ni pamoja na umaskini wa kupindukia ambao
huwafanya wasichana wengi hususan wa vyuo vikuu kujiingiza kwenye biashara ya
kuuza miili.
Alisema sababu nyingine ni baadhi ya watu ambao wameshajitambua kupata
maambukizo ya Ukimwikuueneza kwa makusudi, ulevi wa kupindukia, matumizi ya
dawa za kulevya pamoja na vijana wengi kutokuwa na kazi za kufanya na hivyo
kujiingiza kwenye biashara za ngono.
"Kwa sasa wananchi wengi hawaogopi tena Ukimwi, wanaona ni hali ya
kawaida lakini sisi kama shirika tumekuwa tukijitahidi kutoa elimu hasa kwa
vijana kwani kama hatutakuwa makini tutaipoteza nguvu kazi ya taifa hapo
baadaye," alisema.
"Sheria ya Ukimwiinasema mtu ambaye atabainika kuambukiza ugonjwa
huo kwa makusudi ashtakiwe, sasa tunaomba ifanye kazi na Serikali iweke mkazo
katika hili, ihakikishe wale wote watakaobainika kukiuka sheria hii
wanachukuliwa hatua kali za kisheria," alisema.
Hivi karibuni Mkuu wa
Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, akizungumzia ongezeko la maambukizo ya
ugonjwa wa Ukimwikwa mkoa huo, alisema imeonekana kupanda mara dufu, hivyo
kuwataka wananchi mkoani humo kubadili tabia na kuepuka ngono zembe.
No comments:
Post a Comment