Na Veronica Modest, Musoma
MOJA ya changamoto inayosababisha Mkoa
wa Mara kuendelea kuwa kinara sugu wa ugonjwa wa malaria ni kutokana na
wananchi kuwa na imani potofu juu ya matumizi ya dawa za malaria pamoja na
matumizi mabaya ya vyandarua wakati wa kulala.
Wakichangia
hoja ya namna ya kudhibiti ugonjwa huo katika Mkoa wa Mara juzi katika kikao
cha wadau wa malaria wadau hao walisema kuwa kuna kila sababu ya kutafuta njia
sahihi ya kupambana na ugonjwa huo kwani Mkoa wa Mara umeonekana kuwa tatizo
kubwa.
Akiwasilisha
mada yake mbele ya wadau hao Mratibu wa kampeni ya unyunyiziaji wa dawa ya
kutoka nyumbani, Yusufu Mwita alisema kuwa mkoa umezidi kuwa kinara wa ugonjwa
huo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kutokana na wananchi kuwa na imani potofu juu
ya dawa za malaria pamoja na elimu duni.
Alizitaja
sababu za mikoa mingine kufanikisha kampeni hiyo kuwa ni pamoja na mwitikio
mzuri wa matumizi mazuri ya tiba sahihi ya dawa za malaria,matumizi ya
vyandarua wakati wa kulala na ushirikiano mzuri wa wananchi katika zoezi zima
la unyunyiziaji wa dawa ya ukoka majumbani.
Mwita alisema
kuwa Mkoa wa Mara unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizo ya ugonjwa
huo kwa asilimia 25.6 mwaka 2012 na asilimia 30.5 kutoka mwaka 2007 huku Mkoa
wa Kagera ukipunguza maambukizo hayo kwa asilimia 8.5 mwaka 2012 na asilimia
41.2 kutoka mwaka 2007.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa
alisema kuwa licha ya juhudi mbalimbali za wadau na taasisi mbalimbali
kujitokeza katika kupambana na ugonjwa wa malaria lakini juhudi hizo
hazionekani kuleta maendeleo kama mikoa mingine inavyoleta mabadiliko katika
kupunguza tatizo hilo.
Tuppa alisema kuwa umefika wakati sasa
malaria itangazwe kuwa ni tatizo kwa mkoa wa Mara hivyo liboreshwe kwa kila
wilaya kukaa na kujadili ili kuhakikisha wanatoka na mpango mkakati wa
kupambana na ugonjwa wa malaria.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Tarime, John Henjewelle alisema kuwa moja ya mambo yanayosababisha ugonjwa huo
kuendelea kuwa sugu katika mkoa wa Mara ni pamoja na uchafu kwa kuwa watu
waliowengi hawazingatii suala la usafi wa mazingira katika maeneo yanayozunguka
makazi yao.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Elias Goroi
alisema kuwa ili kufanikisha kazi hiyo ni lazima ushirikishwaji wa wadau pamoja
na wahusika wa maeneo uwepo katika kutoa elimu kwa wananchi wa maeneo husika
hali ambayo itasaidia katika kumwondoa hofu mwananchi wa kawaida na hivyo kazi
hiyo kukamili
No comments:
Post a Comment