12 August 2013

WANANCHI WAIPA POLISI MTIHANI MZITONa Raphael Okello, Bunda.
WANANCHI wa Kata ya Balili wilayani Bu n d a mk o a n i Mara wamelitaka Jeshi la Polisi wilayani humo kuwakamata wahalifu ambao taarifa zao zinawasilishwa kwa jeshi hilo.Walisema endapo jeshi hilo litaendelea kuwakumbatia wahalifu wananchi hao watajichukulia sheria mkononi kwa kuwaua wahalifu hao.

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Polisi Jamii katika mkutano maalum ulioitishwa ili kukabiliana na uhalifu katika Tarafa ya Serengeti wilayani humo.Hata hivyo Mratibu wa Polisi Jamii Tarafa ya Serengeti, Inspekta Hamza Dongwa alisema taarifa zote za uhalifu zinazofikishwa polisi zinafanyiwa kazi.
Dongwa alifafanua kuwa utawala wa sheria ni suala la muhimu hivyo Polisi Jamii inapaswa kufanya mambo yake kwa kuzingatia pia sheria inayolinda halmashauri husika.
Aliwaonya wananchi kutojichukulia sheria mkononi mpaka hapo vyombo vya kutafsiri sheria vimemtia mtuhumiwa hatiani.Alisema mara nyingi wananchi wanawataja wahalifu lakini wanashindwa kutoa ushahidi katika vyombo vya kutafsiri sheria jambo linalofanya watuhumiwa hao kutopatikana na hatia.  

No comments:

Post a Comment