12 August 2013

MAGHEMBE AWAONYA WATUMISHI WANAOKIMBILIA TAKUKURU



Na Martha Fataely, Moshi
SERIKALI imewa o n y a wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na taka mjini Moshi (MUWSA) kutoikaribisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika mamlaka hiyo na badala yake wapeleke malalamiko yao katika bodi ya mamlaka.Waziri wa Maji, Prof.Jumanne Maghembe alisema kuripoti malalamiko yao kwa taasisi hiyo au Jeshi la Polisi ni kuidharau bodi pamoja na ofisi yake kwamba imeshindwa kutatua kero zao.

"Msiite TAKUKURU wala polisi hapa, ipo menejimenti, bodi na chama cha wafanyakazi, mkishindwa kabisa njooni wizara ya maji kwani haiwezekani taasisi hizo zikawa ndiyo mabosi wenu, atakayekiuka nitamfukuza kazi," alisema.Kauli ya Waziri Maghembe inafuatia mamlaka hiyo kwa kipindi cha miezi michache iliyopita kukumbwa na migogoro ya mara kwa mara huku baadhi ya watumishi wakihojiwa na TAKUKURU na kesi nyingine zikifikishwa mahakamani.
M b a l i n a h i l o S e r i k a l i imeitaka ofisi ya maji bonde la Pangani(PBWO) kutotoa vibali vya uchimbaji visima kwa wawekezaji wa mashamba makubwa ya kahawa na badala yake kazi hiyo waiachie mamlaka ya Majisafi na taka mjini Moshi (MUWSA).Kauli hiyo inafuatia taarifa ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo kumueleza waziri kuwapo kwa uchimbaji wa visima kwa wawekezaji binafsi katika mashamba ya kahawa karibu na chanzo cha chemichemi ya Nsere na kusababisha upungufu wa maji katika chanzo hicho.
Akizungumzia jambo hilo,Prof. Maghembe alitaka PBWO kuipa MUWSA jukumu la kuchimba visima hivyo, kwani ndani ya manispaa ya Moshi ni eneo la usambazaji la mamlaka hiyo, hivyo ni vyema kama kuna ulazima wa kuchimba maji hayo ipewe mamlaka ifanye kazi hiyo."Hili jambo sikubaliani nalo hata kidogo, PBWO vibali mlivyotoa vinatosha, msitoe tena kibali vya kuchimba visima ndani ya eneo la mamlaka, kama mtaona ni lazima wasilianeni nami, au waelezeni MUWSA kama wakisema hawawezi kumhudumia huyo mwekezaji ndiyo ifanyike vinginevyo,"alisema.
Prof. Maghembe alisema hayo wakati akizindua bodi mpya ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na taka mjini Moshi(MUWSA) ingawa pia alisisitiza umuhimu wa mamlaka za maji kutotanguliza suala la kuwakatia wateja huduma hiyo bali kuwaelimisha na kabla ya uamuzi wa kusitisha huduma.Wajumbe wa bodi hiyo ni Mwenyekiti, Shally Raymond, Makamu Mwenyekiti Prof.Faustine Bee, Katibu Cyprian Luhemeja, wengine ni Japhary Michael, Elizabeth Minde, Boniface Mariki, Alfred Shayo, Hajira Mmande, Abdala Mkufunzi na Bernadette Kinabo.
Mapema katika taarifa yake, Katibu Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO), Jacob Olotu alisema kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo 2010/2012 kumekuwapo na upungufu mkubwa wa maji katika vyanzo vya Nsere na Shiri jambo lilisababisha kuwa kwa mgawo wa maji katika mji wa Moshi ingawa sasa umekoma

No comments:

Post a Comment