16 August 2013

WANANCHI KUELIMISHWA MATUMIZI ATHARI ZA MIONZI



 Na Jane Edward, Arusha
TUME ya nguvu za Atomic Ta n z a n i a ime j i z a t i t i kuelimisha wananchi na kutambua matumizi bora na salama ya mionzi hasa katika masuala ya uchimbaji wa madini ya urani hapa nchini.Hali hiyo inatokana na wananchi kutokuwa na elimu juu ya madhara yanayopatikana katika madini hayo na hivyo kusababisha madhara kwa baadhi ya sehemu hapa nchini
.Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi mkuu wa tume hiyo, Profesa Iddy Mkilaha alisema kuwa tume hiyo iko makini kuhakikisha jamii inatambua matumizi bora ya mionzi ikiwa ni pamoja na kujua athari zake zinazoweza kujitokeza katika jamii husika.Aliongeza kuwa kutokana na jamii kutotambua madhara yanayotokana na mionzi hiyo ambapo wengi wao wamekuwa wakijenga maeneo ya makazi karibu na machimbo yanayochimbwa madini ya urani pamoja na madini mengine.
Hata hivyo alisema kwamba tume hiyo tayari imefanya kazi ya kutengeneza kanuni pamoja na kufanya tafiti ambazo zitasaidia kuonyesha hali ilivyo kwa hivi sasa na hivyo hatua itakayofuatia ni kuwaelimisha wananchi juu ya uchimbaji wa madini hayo huku wakishirikiana na wadau wengine.A l i o n g e z a k u w a watakaposhirikiana na wadau hao itasaidia kuwaelimisha jamii inayozunguka maeneo ya uchimbaji wa madini ya urani juu ya uchimbaji salama ikiwa ni pamoja na kuwachukulia sheria wale watakaokiuka taratibu za uchimbaji.
Mkilaha aliongeza kuwa kutokana na malalamiko ya wananchi kuhusu usafirishwaji wa madini ya urani kwenda nje ya nchi alisema zipo baadhi ya nchi ambazo hazitumii silaha za nyuklia na wamewekeana mikataba kwa ajili ya kuwauzia madini hayo.Naye Mwanasayansi wa nyuklia, Denis Mwalongo alisema wananchi wengi wamekuwa wakitoa habari za uongo hasa wanaoishi maeneo ya Mahina na Manyoni ambapo ni moja kati ya maeneo yanayopatikana madini hayo.
Alisema kuwa tume hiyo imejipanga kuhakikisha uchimbaji unakuwa salama bila kumdhuru binadamu ikiwa ni pamoja na kusimamia jinsi ya kutengeneza migodi katika hali ya usalama na kuhakikisha uzalishaji unakuwa wa usalama bila kuleta madhara kwa jamii.Aliongeza kuwa zipo baadhi ya sehemu ambazo yanapatikana madini hayo ambapo ni pamoja na Bahina, Manyoni, Mto mkuju pamoja na maeneo mengi ya bonde

No comments:

Post a Comment