12 August 2013

WAKULIMA WATAKIWA KUIENZI NANENANE


Na Lilian Justice, Morogoro

WAKULIMA nchini w a m e t a k i w a k u t e k e l e z a y a l e waliyofundishwa k i p i n d i c h a ma o n e s h o ya wakulima Nanenane ili kuendeleza kilimo na kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla. Hayo yalielezwa jana na Mtafiti wa mbegu za kilimo kutoka katika Kituo cha Utafiti cha Chollima kilichopo Dakawa mkoani humo, George Iranga, wakati akizungumza na gazeti hili na kudai kuwa kwisha kwa maonesho hayo isiwe chachu ya kuachana na yale ambayo wameelimishwa wakulima
. Iranga alisema kuwa endapo wakulima watayashika yale waliyoelimishwa na watafiti mbalimbali wa kilimo waliokuwa wakionyesha bidhaa zao na kutoa elimu kwenye viwanja vya maonesho ya Nanenane ya Mwalimu Julius Nyerere kutaongeza tija ya wakulima kulima kilimo hifadhi ambacho kina tija kwa wakulima wadogo.

Alisema kuwa maonesho ya wakulima ni ya muhimu kwa Watanzania kwani wananchi wengi wanategemea kilimo kwa ajili ya kuendesha maisha yao. Kwa upande wakulima waliofika kwenye maonesho hayo, Omary Juma na Janipha Amos walisema kuwa maonesho ya wakulima ni ya muhimu kwa wakulima ambao wamekuwa wakitegemea maisha yao kwa ajili ya kujiingizia kipato.

Hata hivyo, wakulima hao walisema kuwa imefikiwa wakati Serikali watilie mkazo maonesho ya wakulima ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wakulima kushiriki maonesho hayo kwani ni muhimu kwa wakulima hususan wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment