Na Rashid Mkwinda, Mbeya
DALILI za kumalizika kwa soko la
Mwanjelwa lililogharimu zaidi ya sh.bilioni 13 ambalo linatarajiwa kutumiwa na
wafanyabiashara wanaokadiriwa 1,000 zinaonekana kugonga mwamba baada ya mkandarasi
aliyekabidhiwa kujenga soko hilo
kuvunja mkataba.Soko la
Mwanjelwa liliungua Desemba 2006 na kusababisha hasara kubwa ambapo
wafanyabiashara waliokuwa wakilitumia soko hilo walihamishiwa katika soko la muda katika
uwanja unaomilikiwa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo nchini (SIDO)
. Hatua ya
mkandarasi huyo Kampuni ya Tanzania Building Works kuvunja mkataba inadaiwa
umetokana na msuguano uliopo baina yake na mmiliki wa soko hilo ambaye ni Halmashauri ya Jiji la Mbeya.Katika kikao
cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo hivi karibuni, wajumbe wa kikao
hicho walihitaji kupewa taarifa za maendeleo ya ujenzi wa soko hilo
ambao tangu kuanzishwa kwake limekuwa likikumbana na malumbano ambapo mkataba
wa awali wa soko hilo
ulitakiwa kuishia mwaka 2010.
Kwenye kikao
hicho Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga alimzuia Kaimu Mkurugenzi wa Jiji,
Dkt.Samwel Lazaro kutoa taarifa za maendeleo ya ujenzi wa soko hilo kwa kile kilichoeleza kuwa kinaweza
kuibua maswali mengi kutoka kwa madiwani ambao walihitaji kupewa taarifa hizo.Imeelezwa kuwa
msuguano huo umetokana na mkandarasi kushindwa kukabidhi soko kulingana na
mkataba wake pamoja na kulipwa fedha sh.bilioni 10.6 ambazo ni sehemu ya malipo
ya kati ya sh.bilioni 13 ambazo ndizo gharama halisi ya ujenzi wa soko hilo la kisasa lenye
ghorofa tatu.
Aidha ujenzi wa
soko hilo umedaiwa kuiingizia hasara halmashauri
ya Jiji hilo ambapo katika Kamati ya Bunge
Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) jambo hilo
liliibuliwa na kuelezea sababu za kukwamisha mradi huo wa soko ambalo
likimalizika linaweza kuhudumia wafanyabiashara zaidi ya 3,000.Katika taarifa ya (LAAC) halmashauri
ilimlalamikia mkandarasi kukiuka sheria z a mk a t a b a amb a p o k i l a
alipokabidhiwa fedha kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa soko hilo inadaiwa kuwa
alikuwa akitumia fedha hizo kwa kuendeleza miradi mingine inayoendeshwa na
kampuni hiyo maeneo mengine. Awali ujenzi wa soko hilo ulitarajiwa kutumia jumla ya miezi 18
baada ya kuanza kutekelezwa kwa mradi huo Februari 25, mwaka 2010 na kukamilika
Agosti 25, mwaka 2011.
Pamoja na mkandarasi huyo kushindwa
kutekeleza mradi huo kwa wakati, Halmashauri ya Jiji ilimpa muda wa ziada kwa
awamu tatu za wiki 20 ambapo alishindwa kukamilisha hadi Juni 19, mwaka huu
alipoandika barua ya kuvunja mkataba.K w e n y e b a r u a y e n y e
kumbukumbu SAM/828/RET ya Julai 19, 2013 inamtaarifu mmiliki (Halmashauri ya
Jiji) kusudio lake la kuvunja mkataba kwa kile alichodai kunyimwa nyongeza ya
muda wa ziada wa miezi 9 ili amalizie asilimia 80 ya ujenzi wa soko hilo na kulikabidhi.
Kwa upande wake Halmashauri ya Jiji
iliridhia ombi la kuvunjwa kwa mkataba wa ujenzi wa soko hilo kwa barua yenye kumbukumbu namba
MD/MM/MBEYA/152/2013 ya Julai 25 na kueleza kuwa inachokisubiri ni taratibu za
kisheria ili kukubali kuvunja mkataba huo.Katika sehemu ya barua ya halmashauri
ya jiji imeeleza hatua zilizochukuliwa baada ya muda wa makubaliano kumalizika
Julai 25 ambapo Halmashauri ilipokea utaratibu wa hatua zinazoendelea wakati wa
uvunjaji wa mkataba kutoka kwa mkandarasi kutakiwa kuweka walinzi eneo la
ujenzi ili kulinda mali
zisitoroshwe.
Imeelezwa kuwa hatua ya Halmashauri
kusitisha mkataba wa ujenzi unaweza kuiongezea gharama halmashauri ambapo
italazimika kutumia ziada ya sh.bilioni 3 ikiwa ni ongezeko la gharama halisi
ya sh. bilioni 6 za kumalizia mradi huo.
Ongezeko la gharama kwa Halmashauri ya
Jiji itatokana na kutangaza upya zabuni ya kumpata mkandarasi mpya
atakayechukua kazi ya kumalizia asilimia 20 ya ujenzi iliyobaki.
Hasara nyingine ambayo itaigharimu
halmashauri ya Jiji baada ya kukubali kuvunjwa kwa mkataba na kumtafuta
mkandarasi mpya ni pamoja na kumlipa mkandarasi mshauri wa kampuni ya MD ya
Jijini Dar es Salaam
kiasi cha sh.bilioni 1.2.
Inaelezwa kuwa hali hiyo i t a s a b a
b i s h a Ha lma s h a u r i kupangisha wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa
katika soko hilo ili kupata fedha za kufidia ongezeko la gharama za kumalizia
ujenzi wa soko hilo na kuwanyima fursa wafanyabiashara ambao ni wahanga wa soko
lililoungua.
No comments:
Post a Comment