Rachel
Balama na Anneth Kagenda
SIKU
chache baada ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini kudai jeraha
alilonalo katika bega la kulia limetokana na risasi aliyopigwa na polisi mkoani
Morogoro, baadhi ya Waislamu nchini wametoa tamko la kumtaka Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu mara moja
.Msimamo huo
umetolewa Dar es Salaam
jana katika kongamano la Waislamu ambalo lilifanyika katika Uwanja wa Mwembe
Yanga.Akizungumza
katika kongamano hilo
ambalo lilihudhuriwa na mamia ya waumini wa dini hiyo, mmoja wa viongozi wa
jumuiya hiyo Shekhe Kondo Juma Bungo, alisema Waislamu wanatoa muda kwa Dkt.
Nchimbi kujiondoa katika nafasi hiyo.
Alisema, mbali
na Dkt. Nchimbi, walisema Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Faustine
Shilogile, anapaswa kukamatwa na kufikishwa mahakamani wakidai ndiye mhusika
mkuu wa kupanga mikakati ya kumdhuru Shekhe Ponda.“Askari
aliyempiga risasi Shekhe Ponda na Kamanda ambaye alisimamia suala zima la
uvamizi kwa kiongozi wetu, wote wanapaswa kuwajibishwa... tunataka iundwe tume
huru ya uchunguzi badala ya timu iliyoundwa na polisi,” alisema.
Al i o n g e z
a k uwa , k ama maazimio hayo yatapuuzwa na wahusika pamoja na Serikali
kushindwa kuchukua hatua stahiki, itakuwa mwanzo na mwisho wa historia ya Tanzania.“Kitakachotokea
baada ya hapo, Serikali itaona mwanzo tu lakini haitajua mwisho wake...Wais
lamu nchi nzima
watafanya maandamano, polisi wanategemea kupandishwa vyeo au kupewa posho
nyingi pale yanapotokea matatizo ya Waislamu.“Kwa sasa hali
inavyoonesha watapandishwa vyeo kwa uchungu kwani Waislamu hatutakubali,”
alisema Shekhe Bungo na kusisitiza kuwa, Shekhe Ponda ana thamani kubwa sana kwa Waislamu.
Shekhe Bungo alilihadharisha Jeshi la
Polisi kuacha kuwatisha Waislamu na kuongeza kuwa, Serikali
isije kuwalaumu kwa kitakachotokea kama madai yao hayatatekelezwa.Aliwataka Waislamu popote walipo, kutoa
adhabu palevion gozi au wanachama wa Cha maChaMapinduzi (CCM),wa
napoingiamisikitinina kufan yakampeni zakuombawachaguliwe katika uc haguzi uja
o.
Tamko la
CUF
Katikahatuanyingine,
Chamacha Wana nchi (C UF), kimelitaka Jeshila Polis inchin i,limuach ie Shekh
eP ondaa wezeku endeleanamatibab ukatika Taasisi ya Tiba ya Mifupa(M OI).
Chama hicho kimese ma kite ndoalichofanyiwaS
hekhePondacha kuon dolewaMOI wakat ih ali yakekiafya ha ijatengemaa,s
ichakibinadamubal ich akinyam a.
Mwenyek itiw ac hamahicho Taifa,Pro
fesaIbrahim Lipum ba, aliyase mahayo Dar esS alaamjanawak ati akizungumza na
waandishi wahabari.
"Kaulizaviti shonaub abeunaofany
wa naKam an dawa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman
Kova, vinachochea hasira na jazba za wananchi wengine wakiamini kuwa, jeshi
hilo lina lengo la kumuua Shekhe Ponda badala ya polisi kujenga amani, wao wanaibomoa,"
alisema.
Prof. Lipumba alisema, jeshi hilo limeshindwa kufanya
kazi kwa weledi ndio sababu ya kuongezeka vitendo vya uhalifu na tuhuma nyingi
kwa baadhi ya polisi ambao wanashirikiana na wahalifu.
"Polisi wetu wameweka pembeni kazi
yao ya kupambana
na uhalifu... wanapoteza wakati mwingi na raslimali kumshughulikia Shekhe Ponda
hivyo nawaomba Watanzania wote tudai jeshii lenye weledi na
linalowajibika," alisema.
Alisema CUF kinaungana na Watanzania
wote kulaani vikali kitendo alichofanyiwa Shekhe Ponda, kumfungulia mashtaka na
kumuondoa MOI alipokuwa akipatiwa matibabu bila taarifa na kumpeleka gerezani
Segerea.
Aliongeza kuwa, jeshi hilo
ndio chanzo cha wananchi kuvunja amani ya nchi ambapo juzi mchana, alikwenda
Segerea kumuona Shekhe Ponda ambapo Mkuu wa gereza hilo alimpa ushirikiano mzuri uliofanikisha
amuone na kuzungumza naye.
" Ta y a r i S h e k h e P o n d a
amepelekewa dawa zake gerezani na amepewa huduma za tiba zinazoweza kupatikana
katika gereza hilo,"
alisema Prof. Lipumba na kuongeza kuwa, taarifa alizonazo X-ray imeonesha
risasi aliyopigwa imepita karibu na mfupa ambao umepasuka.
Alisema hali ya Shekhe Ponda inaendelea
vizuri ukilinganisha naawal i baad ayaku fikishwa ger ezanikwanian awe
zakutembeamwenyewe, anafahamu kamili na waliweza kutaniana na mkuu wa gereza
ambaye alimhakikishia kupata huduma nzuri.
Prof. Lipumba aliongeza kuwa, anazo
taarifa kuwa Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linataka kumhoji daktari
aliyemtibu Shekhe Ponda, siku alipopigwa risasi.
"Inasikitisha kwamba polisi
hawajapitia Taasisi ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), ili iombe kibali
cha kufanya hivyo badala yake wanataka kumsulubu daktari kwa kosa la kumtibu
Shekhe Ponda jambo ambalo linashangaza," alisema.
Aliongeza kuwa, CUF inataka Serikali
iunde tume huru ambayo itaongozwa na Jaji ili kuchunguza tukio la kupigwa
risasi Shekhe Ponda, askari aliyempiga na waliompa amri ya kufanya hivyo
wafikishwe mahakamani na kumfutia kesi ya uchochezi.
Shekhe
Ponda alipata mkasa huu Agosti 10 mwaka huu mkoani Morogoro muda mchache baada
ya kushiriki katika Kongamano la Baraza la Eid.
No comments:
Post a Comment