19 August 2013

SERIKALI ITUMIE MASHINE ZA KIELEKTRONIKI KAMATI Na Anneth Kagenda
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Serikali za Mitaa na Kamati ya Bajeti, zimeitaka Serikali itumie mashine za kieletroniki kutokana na ukosefu wa taarifa sahihi kuhusu deni la Taifa ambapo upo umuhimu mkubwa wa kukutanisha wadau kama Benki Kuu (BoT) na hazina.Mwenyekiti wa PAC, Bw. Zitto Kabwe, aliyasema hayo jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kuongeza kuwa, hayo ni kati ya maazimio yaliyopitishwa na kamati hizo.

Al i s ema k ama t i h i z o zimeishauri Serikali kuunda c h omb o h u r u amb a c h o kitasimamia deni la Taifa ambapo Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, haiweki uwazi wa kutangaza umiliki wa mali za viongozi.Bw. Kabwe aliongeza kuwa, hali hiyo inasababisha viongozi kutoweka wazi mali wanazomiliki hivyo ni rahisi mtu kuzushiwa umiliki wa mali usio wa ukweli.
"Ni vyema Sekretarieti ikafanya utafiti juu ya umiliki wa mali kwa viongozi wa Umma na kuweka taarifa hizo katika tovuti ya Sekretariati ili kuwawezesha wananchi kuona mali zinazomilikiwa na viongozi wao.
Aliongeza kuwa, kwa kuwa hivi sasa leseni za udereva zinaweza kuweka kumbukumbu za makosa ya usalama barabarani, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), ikishirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhakikisha askari wa Usalama Barabarani wanatumia utaratibu huo wa kisasa wa kutoza faini na kutoa risiti za malipo za elektroniki.
Alisema kamati zimeridhia maduhuli ya Serikali, yakusanywe kwa kutumia risiti za elektroniki ambapo Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma, yaanze kutumia risiti za eletroniki mara moja kudhibiti upotevu mapato ya serikali.
"Pia tumekubaliana ofisi zote za Serikali zifanye manunuzi yake kwa wafanyabiashara wanaotumia mashine za kielektroniki pamoja na kufanyiwa mabadiliko kwa sheria ya "The Proceeds of Crime Act, 1991".
"Sheria hii tunataka iwekwe kifungu kinachomwezesha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP", kuwa na mamlaka ya kuomba mahakama kufungua kesi ya madai kwa watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi," alisema

No comments:

Post a Comment