06 August 2013

MWANRI ATAKA WAKAGUZI KUCHUNGUZA UBADHIRIFU


NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Benedict Ole Kuyan apeleke timu ya wakaguzi wilayani Kilindi kwenda kuchunguza fedha zilizopelekwa kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Jaila
.Agizo hilo alilitoa baada ya kuonekana hakuna uwiano wa fedha zilizotumika na kazi iliyofanyika.Mwanri aliyasema hayo juzi baada ya kufika kwenye kituo hicho na kukuta fedha zilizotolewa na halmashauri ya wilaya hiyo sh. milioni 35 hazijafanya kazi za kumridhisha, jambo lililofanya kuwaweka kitimoto baadhi ya wakuu wa idara kwenye kituo hicho.
Alisema, kazi kubwa ya majengo mawili yaliyojengwa kwenye kituo hicho ikiwemo jengo la wagonjwa wa nje (OPD), ofisi za madaktari na wauguzi zimefanywa na wananchi huku Shirika la World Vision likitoa vifaa ikiwemo saruji.
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Suleiman Liwowa alipigilia msumari wa mwisho baada ya kusema hata wao kama wilaya wameona kuna 'uchakachuaji' wa fedha hizo na suala hilo wamelifikisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU

No comments:

Post a Comment