MKUUwaWilayayaI gunga mkoani T abo ra,
Eliba rik iKinguamewaasavio ngoziw adini kutojihusish a namasual aya
siasanabadala yake wajengemi singiya kirohokwawaumini ilinchi iendeleek
uwanaamani,anaripoti Abdalla hAmi ri, Igunga
.Ha yoaliyasemamw
ish onimwawikika tika tamas halauzin duzi waalbam u yan yimbozai njili ya,
AnnaNzog iijulikan ayo kwajinalaNjo onitumwimbi e b wana uliof an yikakati ka
ukumbiwaShuleyaMsingi St.Leo the Great uliopo mj ini Igunga.
A lisem a
kuwabaad hiyaviongozi wadiniwameku wawa ki jihusishana masuala yasias anakuacha
kumtumikiaMu nguh ali ambayoina letamfarakano katika shughuli zamae ndeleo.
Aliongezakuwabaadhiyawananchi
wam ekuwa wakitum ia fedha nyingi kwakufanyamamboyasiyompendeza Mungu badala ya
kuwekeza katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kutoa sadaka.
“Ndugu waumini
mliokusanyika katika tamasha hili, leo nimeona niyaseme haya kwani kuna baadhi
ya watu wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kwenda kwa waganga wa kienyeji na
kudanganywa na hatimaye kujiingiza katika vitendo viovu ambavyo vinamchukiza
mwenyezi mungu,” alisema Kingu.
Katika tamasha
hilo lilienda sambamba na harambee ya kuchangia kwaya ya Jerusalemu ya Kanisa
la Moravian mjini Igunga kwa ajili ya kusaidia watoto yatima, wajane na watoto
wanaoishi katika mazingira magumu.
Aidha, katika
harambee hiyo jumla ya sh.milioni 1.4 zilichangwa ambapo mkuu huyo wa wilaya
alichangia kiasi cha sh.650,000.
Naye mlezi wa
Kwaya ya Jerusalemu ya Kanisa la Moravian mjini Igunga, Nyanza Sulwa aliwaomba
viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa liendelee kuwa na amani.
Alisema kuwa ili nchi izidi kuwa na
amani ni vyema wananchi waendelee kumuomba Mungu kwani kumekuwa na viashilia
mbalimbali vya uvunjifu wa amani ambapo watu wamekuwa wakimwagiwa tindikali na
kupigwa risasi pasipo makosa yoyote.
Kwa upande wake, Mchungaji wa Kanisa la
Moravian mjini Igunga, Isaya Misayo aliwataka waimbaji wa nyimbo za injili
kutotanguliza masilahi mbele na badala yake wafanye kwa ajili ya kumtumikia
Mungu.
Aliongeza kuwa kumekuwa na baadhi ya watu wanaotumia mambo ya dini
kwa nia ya kujipatia vipato vyao binafsi na kuwaasa waachane na tabia hizo.
No comments:
Post a Comment