Na Mwandishi Wetu
UTOAJ I h u d uma b o r a umetajwa kuwa
ndiyo kipaumbele cha kwanza kwa wateja wa benki ya Exim na kwamba tayari
imeanzisha mfumo wa kupunguza foleni katika matawi yake ikiwa ni moja ya
mikakati ya kuboresha huduma kwa wakati.
Hayo yalisemwa na meneja wa huduma kwa
wateja wa benki hiyo, Frank Matoro, wakati wa maadhimisho ya miaka 16 tangu
ianze kutoa huduma hapa nchini.Alisema utoaji wa huduma bora ni
kipaumbele kikubwa kwa benki yake na kwamba tayari benki imeshaanzisha mfumo wa
kupunguza foleni katika matawi yake.
“Pia tumeanzisha huduma za kisasa ya
kuwasiliana na wateja kupitia mtandao ambayo inajulikana kama Online Chat
Service, kwa ajili ya wateja wetu kuwasiliana na wawakilishi wa benki kupitia
mtandao watakaosaidia kutatua matatizo yao
mbalimbali kwa wakati,” alisema Matoro.
Akizungumza wakati wa sherehe ya
maadhimisho hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, ofisa mtendaji mkuu wa
benki hiyo, Dinesh Arora, alisema benki yake imejikita katika utoaji wa huduma
za kibenki za kipekee ikiwa na lengo la kuziba pengo la wasiofikiwa na huduma
hiyo nchi nzima.
Alisema maadhimisho ya miaka 16
yamekuja yakiambatana na mafanikio ya benki hiyo kwenye sekta ya kibenki Afrika
kutokana na kuorodheshwa kwenye tuzo za Benki Bora Afrika, zilizofanyika jijini
Marrakesh, Morocco.
“Tutaendelea na jitihada zetu za kutoa
huduma baada ya kumaliza miaka 16 yenye mafanikio makubwa,” alisema na
kuongeza;“Mafanikio
yetu katika kipindi hiki yametokana na dhamira yetu ya kutoa huduma za kibenki
za kipekee zitokanazo na wafanyakazi, makini na wateja wetu waaminifu.”
No comments:
Post a Comment