Na Rehema Maigala
MW E N Y E K I T I wa
Kama t i y a W a n a w a k e mashambani na Kilimo (TPAWU), Patricia K i s h i m
b a a m e s e m a hawakuridhishwa na kima cha chini cha mshahara
kilichotangazwa na Serikali sh 100,000
. Akizungumza katika kikao cha utendaji cha wanawake alisema
walijadili kuhusu kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wa mashambani na
kuona haufai kulingana na maisha yalivyo sasa. "Hatukuridhishwa na kima hicho cha mshahara kulingana na
maisha ya sasa yalivyo hivyo hivi sasa tumeaandaa mapendekezo kwa ajili ya
kuyapeleka serikalini kwa ajili ya kutuongezea kiasi hicho cha pesa,"
alisema Kishimba.
Aliongeza kuwa Serikali inatakiwa kuangalia upya kima hicho cha
mshahara ili nasi tuweze kufanya kazi kwa bidii na kwa tija zaidi. Naye Mwenyekiti wa Taifa wa (TPAWU), Jaicy Kayera alisema
watafanya mkutano mkuu wa chama hicho ambapo kwa hivi sasa itakuwa ni mara ya
kwanza kwa chama hicho kufanya mkutano huo.
Alisema lengo la kikao hicho ni kuangalia kazi za chama tangu
miaka saba iliyopita kuangalia mapitio ya katiba ya chama kwani wa n a c h ama
wa l i t a k a katiba ya sasa iboreshwe na kuangalia hali halisi ya wafanyakazi
na sheria za kazi zilizopo. Hata hivyo, Kayera alisema chama chao kina mikutano mikuu
miwili ambayo ni mkutano mkuu na mkutano wa kazi
No comments:
Post a Comment