Na Grace Ndossa
SHIRIKA la Viwango nchini (TBS) limesema mafuta ya kula aina
ya OKi yanaruhusiwa kusambazwa kwenye soko la ndani baada ya kubainika hayana
madhara. Uamuzi huo unatolewa zikiwa zimepita siku kadhaa, TBS kutangaza
kwa umma kuwa mafuta hayo ambayo yanazalishwa nchini Malaysia hayafai kwa
matumizi ya binadamu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na
kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo jana, Joseph Masikitiko ilieleza
kuwa uchunguzi waliofanya kwa kushirikiana na Tume ya Ushindani (FCC)
waligundua kuwa mafuta hayo hayana matatizo kiafya.
Taarifa hiyo, ilieleza kuwa baada ya uchunguzi wa kina kuonesha
hayana madhara wamemtaka mzalishaji wa mafuta ya OKi kuteua wakala ambaye
atahusika na uingizaji na usambazaji wa mafuta hayo nchini. Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, mzalishaji anatakiwa kuuza kwa
wakala mafuta ya ujazo wa lita 10-20 tu katika vifungashio vya madumu ya
plastiki.
"Mafuta ya Oki yanaruhusiwa kusambazwa na kuuzwa kwenye soko
la Tanzania baada ya uchunguzi yakinifu uliofanywa na shirika kwa kushirikiana
na Tume ya Ushindani (FCC), mzalishaji wa mafuta hayo na kubaini tatizo ni mafuta
bandia yanayoingizwa nchini kupitia njia za panya na kuuzwa na wafanyabiashara
wasio waaminifu," alisema Masikitiko.
A l i s e m a , T B S k w a kushirikiana na Tume ya Ushindani
watahakikisha mafuta ya OKi yanaingia nchini kwa utaratibu uliokubalika na
yatapewa alama ya ubora. Pia alisema, mafuta ya Oki ya ujazo wa lita moja hadi tano
ambayo yamepimwa na kukutwa hayakidhi viwango hayaruhusiwi kuuzwa na ruhusa
hiyo haitahusu mafuta ya kupikia ya Viking na ASMA, kwa kuwa mpaka sasa
wazalishaji na wafanyabiashara wa mafuta hayo hawajapatikana wala kujitokeza
ili kushughulikia matatizo yanayohusu bidhaa zao.
No comments:
Post a Comment