01 August 2013

TBF YAPIGIA MAGOTI WADHAMINI



Na Mosi Mrisho
SHIRIKISHO la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), limeomba wadhamini kujitokeza ili kuwasapoti katika michuano ya Taifa Cup, itakayofanyika Novemba 30, mwaka huu.Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Msaidizi wa TBF, Michael Maluwe alisema michuano hiyo itafanyika jijini Mbeya hadi Desemba mwaka huu
. Maluwe alisema hadi hivi sasa timu zitakazoshiriki katika michuano hiyo bado hazijapata wadhamini ndiyo maana wanaomba kampuni, taasisi na wafanyabiashara kujitokeza na kuwasapoti.Maluwe alisema lengo hasa la mashindano hayo ni kutoa vipaji na kukuza mchezo huu hapa nchini. "Lengo la michuano hii ni kukuza na kuibua vipaji, kwani mchezo huu unazidi kukua kwa kasi hapa nchini," alisema.
Aliongeza kuwa vijana wengi nchini, hasa wa shule wametokea kuupenda mchezo huu hivyo kwa mashindano haya, tunaamini tutazidi kuongeza wachezaji na hata mashabiki.Pia ameitaka mikoa mbalimbali nchini kuhamasisha vijana kuchukua fomu za usaili kwenye timu, ili waweze kushiriki michuano hii.

No comments:

Post a Comment